Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,akizungumza wakati wa kikao cha tasmini juu ya maeneo na migodi ambayo wamezungukia Mkoani Geita. |
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mara Joyce Sokombi akiandika baadhi ya point zilizokuwa zikizungumzwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo. |
Wajumbe wakifuatilia Kikao. |
Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,akitoa maagizo kwa wanufaika wa Ruzuku. |
Kaimu Kamishna wa Madini ,Mhandisi Ally Samaje akimwakikishia Mwenyekiti wa kamati hiyo kutekeleza maagizo ambayo ameyatoa. |
Naibu Katibu Mkuu Prof,James Mdoe,akisisitiza kwa wachimbaji ambao wamepatiwa Ruzuku mpango wa kuwazungukia wote. |
Mwenyekiti wa halamshauri ya Mji wa Geita,Lernad Kiganga Bugomola akijitambulisha kwa wajumbe. |
Meneja Mahusiano ya jamii mgodi wa GGM ,Manase Ndoloma akielezea namna mgodi huo umekuwa ukichochea maendeleo kwa wananchi Mkoani Geita. |
Kamati
ya Bunge ya Nishati na Madini imeitaka wizara hiyo na Stamico
kuangalia ubia na leseni ya mgodi wa Buckreef Gold Company Limited
uliopo Rwamgasa ambao kwa muda umekuwa ufanyi kazi za uchimbaji huku
kuna wachimbaji wadogo wamekuwa wakihitaji kufanya shughuli za
uchimbaji kwenye maeneo ambayo yameshikiliwa na mwekezaji .
Akizungumza
baada ya ziara ya siku nne Mkoani Geita,Mwenyekiti wa kamati hiyo
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,amesikitishwa na
mwekezaji wa Backreef kushikilia eneo kubwa huku kuna baadhi ya wananchi
wanaidai kampuni hiyo fedha nyingi.
“Kuna
eneo la Backreef tunakuomba sana na tunaitaka Wizara na Stamico muende
mfanye haraka sana muangalie patna ship zenu mnaleta wabia ambao kwa
sehemu kubwa ni wajanja wajanja tu hakuna wanachofanya eneo wamelikalia
wachimbaji wadogo wadogo mngewapatia eneo hilo ingekuwa na maana kubwa
zaidi kuliko mnampatia mtu mmoja mgeni anashika eneo kubwa leseni 13 kwa
miaka yote hakuna anacho fanya halafu tunaona sisi watanzania
tumezidiwa akili na mtu mmoja hilo halikubaliki lakini msimamie kuna
madeni ambayo watanzania wanamdai ahakikishe anayalipa”Alisema Biteko.
Sanjari na hayo Mwenyekiti Biteko,ameitaka wizara kuhakikisha fedha za ruzuku zinawafikia
walengwa na kwamba pesa hizo zisipelekwe kwenye matumizi ambayo ni kinyume na shughuliza za uchimbaji.
walengwa na kwamba pesa hizo zisipelekwe kwenye matumizi ambayo ni kinyume na shughuliza za uchimbaji.
Hata
hivyo kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Madini ,Mhandisi Ally Samaje
amemwakikishia Mwenyekiti wa kamati hiyo kutekeleza maagizo ya kamati
ikiwa ni pamoja na fedha za ruzuku kufanya kazi ambazo zinatakiwa.
Naibu
Katibu Mkuu Prof,James Mdoe,amesisitiza kuwa kwa wachimbaji ambao
wamepatiwa Ruzuku kuna mpango wa kuwazungukia wote na kujua namna
ambavyo wametumia fedha hizo na kwamba hoja zote zilizozungumza
watazijibu kwa maandishi kujua maamuzi ambayo wameyachukua kutokana na
fedha za ruzuku
No comments :
Post a Comment