Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6
kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya
Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana
Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu
Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi
Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6
kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya
Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana
Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu
Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni
Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali
Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya
Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar
Behranwala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu
ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini
India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa
Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin
Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam
mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu
ya Mabohora nchini, Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa
Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa(kulia).
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo
kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge
akifafanua jambombele ya waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa kambi
ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29
Machi katika Taasisi hiyo ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na
Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia
ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu
Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea
Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Katikati ni
Mwakilishi Mkazi wa Madhebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai
na Daktari Bingwa wa Upandikizaji wa Mishipa kutoka Hospitali ya Saifee
ya Mumbai, India Dkt. Yunus Loya.
Daktari Bingwa wa kupandikiza
mishipa ya damu kwenye moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini
India Dkt. Yunus Loya akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari
kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na
Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia
ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu
Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea
Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kutoka kushoto
ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini, Sheikh Tayabali
Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa
(kulia).
Daktari wa anayeshughulikia
maumivu na usingisi wakati wa upasuaji kutoka India Dkt. Shilpa Bhojraj
akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu
ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini
India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa
Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin
Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam
mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu
ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa
Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt.
Bashir Nyangasa.
Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa
moyo kuzibua njia mbili, Athumani Waziri akielezea namna alivyofarijika
baada ya kupata matibabu hayo wakati wa kambi ya siku tatu ya upasuaji
wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mezi Machi katika Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI
walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktari hao
wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora
Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt.
Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13,
Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini
Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka
Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
kuhusu aina ya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na
kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba ( CABG-Coronary Artery
Bypass Graft) aliyofanyiwa mgonjwa Vinod Bhaggan (katikati) wakati wa
kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26
hadi 29 mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini
India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa
Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin
Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam
mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Sheikh Tayabali
Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya
Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala.
Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa
kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo
iliyoziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) Vinod Bhaggan akielezea
namna alivyofarijika baada ya kupata matibabu hayo wakati wa kambi ya
siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29
mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo
madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India.
Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa
Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb
kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema
tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya
Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar
Behranwala (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Daktari Bingwa wa
Upasuaji wa Moyo wa JKCI Dkt. Bashir Nyangasa na Mkurugenzi wa Upasuaji
wa JKCI Dkt. Peter Kisenge (katikati) mara baada ya kumaliza kambi ya
siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es
Salaam, ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka
nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi
Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal
Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar
es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.
Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akipokea zawadi kutoka kwa
Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Tanzania Sheikh
Tayabali Hamzabhai (wapili kushoto) mara baada ya kuzungumza na
waandishi wa habari kuhusu
kumalizika kwa kambi ya siku tatu ya upasuaji
wa Moyo katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai
nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala(kulia) na Dkt. Hussein Hassanali
wa JKCI.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
……………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuli amepongezwa kwa kuiwezeshaTaasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) kufanya upasuaji wa kihistoria tangu kuanzishwa
kwake.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa
Moyo Dkt. Bashir Nyangassa wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari
bingwa wa moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai nchini India
waliosaidia kufanikisha upasuaji huo wa kuvuna mishipa ya damu mguuni
na kupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba (CABG-Coronary Artery
Bypass Graft) kwenye moyo .
Upasuaji huu uliwahusisha
madaktari 6 toka Hospitali ya Saifee umesaidia kuwaongezea ujuzi
wataalamu wa Taasisi hiyo na kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika
kuwasafirisha nje wagonjwa ili waweze kupata matibabu.
“Kama wagonjwa hawa wangeenda
kutibiwa nchini India Serikali ingelipia zaidi ya shilingi bilioni 2.1
kama gharama za matibabu” Alisisitiza Dkt. Nyangassa. “
Akizungumzia upasuaji mwingine
uliofanyika kwa wagonjwa 8 Dkt. Nyangassa amesema kuwa ni upasuaji wa
milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo ilikuwa na matatizo kwa
kuibadilisha.
Kwa upande wa upasuaji wa bila
kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cath Lab tumetoa huduma mbalimbali
za matibabu ya moyo bila kufungua kifua (catheterization) kwa wagonjwa
12 ambao tumezibua mishipa ya damu ambapo mgonjwa mmoja mshipa wake
ulikuwa umeziba kwa asilimia 100” Aliongeza Dkt. Nyangasa.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya nchini India Dkt.
Yunus Loya amesema kuwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete umeonyesha mafanikio makubwa na utakuwa wa kudumu.
Aliongeza kuwa Taasisi ya Moyo ya
Kikwete ina wataalamu wazuri na siku za usoni watakaobobea zaidi na
hivyo Tanzania itanufaika sana na uwepo wa Taasisi hiyo.
Tangu kuanza kwa mwaka huu
Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wake wa nje ya nchi imefanya
upasuaji bila kufungua na kufungua kifua kwa wagonjwa 79.
Mwaka 2016 Kiongozi Mkuu wa
Madhehebu ya Bohara Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal
Saifuddin alifanya ziara yake hapa nchini na katika ziara hiyo kiongozi
huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Dkt. John Magufuli na
kumuahidi kuleta madaktari wa moyo. nchini watakaoshirikiana na
Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na kufanya matibabu kwa
wagonjwa.
No comments :
Post a Comment