Friday, March 24, 2017

DKT KEBWE AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA KILIMO


kereee
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa kikao cha
Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane)
Kanda ya Mashariki
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane)
Kanda ya Mashariki wakifatilia kikao hicho kwa makini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha
Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Masharikikilichofanyika Mkoani Morogoro
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akifatilia kwa makini kikao cha
Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane)
Kanda ya Mashariki kilichofanyika Mkoani Morogoro, Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi, Mwanasha Tumbo akichangia jambo wakati wa kikao cha
Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane)
Kanda ya Mashariki
Na Mathias Canal, Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ameongoza kikao cha

Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane)
Kanda ya Mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani
na Morogoro.
Kikao hicho kilichokuwa na Agenda sita kimefanyika
Katika Ukumbi wa JKT Nane Nane Manispaa ya Morogoro ambapo kwa kauli
moja kimepitisha Agenda zote sita ikiwemo kupitia Taarifa ya Tathmini ya
Maonesho ya Nane Nane 2016 sawia na Taarifa ya Maandalizi ya Maonesho
ya Nane Nane ya mwaka 2017 ambayo Kitaifa yanayotaraji kufanyika Mkoani
Morogoro.
Akizungumza wakati Akifungua kikao hicho Dkt Kebwe
ameitaka kamati inayoratibu shughuli hizo ya TASO kuweka wazi mapato na
matumizi ya fedha wanazozipata kwani kufanya hivyo ni kujenga zaidi
uaminifu kwa wananchi na kujihuisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ili
kukuza uchumi nchini kupitia Kilimo.
Dkt Kebwe alisema kuwa TASO
kutofanya hivyo ni njia mojawapo ya kuzifanya Halmashauri zingine
kutochangia kwa kuhofia fedha zao kutumika pasina weledi uliokusudiwa.
Sambamba na hayo pia amewasihi wadaiwa sugu kulipa madeni yao haraka
iwezekanavyo kwani kufanya hivyo itaongeza ustawi na uimara wa
Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na hatimaye Kilele chake kuwa na Tija
kwa jamii.
Dkt Kebwe amewapongeza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya
waliohudhuria katika kikao hicho ambapo alisema kuwa wanafanya kazi
nzuri na kuonyesha ushirikiano imara katika Maandalizi hayo japo
amesisitiza kuongezwa kwa jitihada za Maandalizi ili Maonesho hayo yawe
na weledi na tija.
Sherehe za Maonesho ya Kilimo Nane Nane
hufanyika kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa
kuwaelimisha watazamaji na hasa wakulima, wafugaji na wavuvi kujifunza
na kupata uzoefu wa teknolojia na mbinu zinazotumika kuongeza uzalishaji
katika eneo la kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Katika Maonesho hayo
mambo muhimu hutawala ikiwa ni pamoja na kuonyesha mazao mbalimbali
sambamba na mifugo mbalimbali kwenye mabanda.
Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewapongeza viongozi wote kwa namna
ambavyo wanashiriki kuandaa Maonesho hayo huku akisema kuwa pamoja na
Halmashauri ya Ubungo kuwa mpya na inaanza kushiriki katika Maonesho
hayo kwa Mara ya kwanza atahakikisha kuwa maonesho yanakuwa na tija
katika mabanda yote yanayoendelea kuandaliwa na Maafisa Kilimo, Uvuvi na
Mifugaji.
MD Kayombo alisema kuwa kupitia Maonesho ya Kilimo
mwaka huu 2017 wananchi watapata fursa ya kujifunza mbinu za ufugaji
kwa kutumia mabanda bora, Uchanganyaji wa vyakula vya mifugo na
ulishaji, Teknolojia bora ya ufugaji wa samaki wengi katika eneo dogo,
Utotoleshaji vifaranga kwa kutumia incubator ya kienyeji na kisasa,
Uhamilishaji wa samaki na Ng’ombe na teknolojia Nyinginezo.
Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe
ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho alizitaja changamoto za
maandilizi za Maonesho ya Kilimo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa
michango kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na kuchelewa kuthibitisha
mialiko kwa wageni walioalikwa kutembelea Maonesho ya Kilimo Nane Nane.

No comments :

Post a Comment