Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Watoto Bi. Margaret Mussai katikati akiongea na waandishi wa habari
hawapo pichani kughusu siku ya kimataifa ya kuzuia ukeketaji kushoto
kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bwana Erasto
Ching’oro na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeley ya Jinsia
Bwana Julius Mbilinyi.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Watoto Bi. Margaret Mussai pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeley ya
Jinsia Bwana Julius Mbilinyi akiongea na waandishi wa habari hawapo
pichani kughusu siku ya kimataifa ya kuzuia ukeketaji .
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeley ya
Jinsia Bwana Julius Mbilinyi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Watoto Bi. Margaret Mussai k akifafanua jambo mbele ya waandishi wa
habari hawapo pichani kughusu siku ya kimataifa ya kuzuia ukeketaji
…………………………………………………………………….
Masuala ya ukatili wa kijinsia
ikiwemo ukeketaji yameendelea kuwa tatizo kwa taifa na ulimwengu mzima
na ili kukabiliana na tatizo hili, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa
kimataifa na kitaifa katika kukabilana na vitendo vya ukatili wa
kijinsia.
Akiongea na vyombo vya Habari
Jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Margaret Mussai
amesema Serikali inalaani na kukemea vikali ukatili kwani unadhalilisha
na kunyanyasa hadhi na utu wa mwanamke na mtoto wa kike akisema jambo
hili halikubaliki.
Aidha aliongeza kuwa ni lazima
jitihada za makusudi zichukuliwe na wadau wote kuhakikisha kuwa
tunashiriki kwa pamoja kuzuia na hatimaye kutokomeza ukatili wa kijinsia
katika jamii zetu, hususan kuzua ukeketaji.
Aidha kulingana na takwimu za
Tafiti ya Idadi ya Watu na Afya (TDHS 2010) inakadiriwa kuwa ukeketaji
kwa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15- 49 ni asilimia 14.6,
hii imepungua kidogo ukilinganisha na asilimia 17.9 mwaka 1996.
Aidha, takwimu hizo kwa mwaka 2015/16 zinaonyesha kiwango cha ukeketaji
kwa wanawake na watoto kimepungua kutoka asilimia 14.6 ya mwaka 2010
hadi kufukia asilimia 10.
Margaret ametaja mikoa
inayoongoza kwa vitendo vya ukeketaji ni Manyara (58%), ikifuatiwa na
Dodoma (47%) na Arusha (41%) akitaja kuwa kupunguwa kwa vitendo vya
ukeketaji kunatokana na kampeni za uhamasishaji, uelewa na kujitambua
kwa wasichana wanaofanyiwa vitendo hivyo, hofu ya kufungwa kutokana na
uwepo wa sheria zinazotekelezwa, hivyo mangariba na wazee wa kimila kwa
kiasi kikubwa wanaamua kuacha mila hii ya ukeketaji.
Aidha Serikali inahimiza
kuendeleza mila zenye manufaa na kujenga utamaduni chanya kwa jamii.
Amewaomba wadau mabalimbali wakiwemo wana habari, mashirika yasiyo ya
kiserikali, Taasisi za dini, sekta binafsi na mamlaka za serikali za
mitaa kuendelea kuongeza juhudi za kuelimisha jamii kuachana na mila
zinazochochea ukeketaji.
Aidha Serikali imetunga sera,
sheria, miongozo na kuandaa mikakati mbalimbali katika jitihada za
kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia,ikiwemo ukeketaji, Sera ya
Wanawake na Maendeleo ya Jinsia (2000) na Mkakati wa Maendeleo ya Jinsia
(2005), Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008). Sheria ya Makosa ya
Kujamiiana -SOSPA (1998) na Sheria ya Mtoto (2009) vyote vikiwa na lengo
la kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katika kuongeza jitihada za
kutokomeza ukeketaji serikali imeandaa Mpango wa kazi wa Taifa wa miaka
mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto
(2017/18-2021/22). Mpangokazi umeanisha maeneo nane muhimu mojawapo ni
la kuondoa mila na desturi zenye madhara. Kupitia mpango huu serikali
imedhamiria kupunguza ukeketaji kwa wanawake kwa asilimia 50ifikapo
mwaka 2022.
No comments :
Post a Comment