Wednesday, February 22, 2017

WASTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ZANZIBAR WAENDELEA KUHAKIKIWA.


1
Baadhi ya Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania wakiwa katika lango la Wizara ya Fedha Zanzibar kwa ajili ya kufanya uhakiki unaoendelea Wizarani hapo.
2
Mmoja kati ya Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania akipelekwa katika chumba cha Uhakiki Zoezi linaloendelea  Wizara ya Fedha Zanzibar.
3
Mhakiki wa Wastaafu Mary akiendelea kufanya kazi ya Uhakiki wa Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Zoezi hilo linaloendelea  Wizara ya Fedha Zanzibar.
4
Baadhi ya Wahakiki wakiendelea na Kazi ya Uhakiki wa Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
5
Mhakiki wa Wastaafu Blandi Shija akimfanyia Uhakiki mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
6
Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali Stanslaus Mpempe akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Uhakiki wa Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Zoezi linaloendelea  Wizara ya Fedha Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

No comments :

Post a Comment