Friday, February 3, 2017

WANAFUNZI KUTOKA SHULE YA SHERIA TANZANIA WAPATA MSASA JUU YA MATUMIZI YA IT KWENYE SHERIA


 




 
 SHERIA
 
Siku ya Jumanne, Januari 31, Dudumizi Technologies alipata wasaa kutoa mafundisho kwa wanasheria wanaosomea mafunzo ya sheria kwa vitendo kwenye shule ya sheria Tanzania (The Law School of Tanzania). Mafundisho hayo yalilenga juu ya njia bora za kutumia ICT kwenye kuongoza taasisi na makampuni ya sheria Tanzania.
Sambamba na matumizi hayo ya ICT, wanasheria hao walipata nafasi ya kujionea programu mpya ambayo ni moja ya product za Dudumizi inayowawezesha kuongeza ufanisi wa ufanyaji kazi zao. Programu hiyo inayoitwa DuLaw siyo tu inawawezesha kuchunga kesi (Case Management), pia inawawezesha kuchunga mafaili, taarifa za mienendo ya kesi, matukio (events), taarifa za kifedha (Invoices), taarifa za wateja, mawasiliano ya wateja na wafanyakazi, kupata ujumbe juu ya taarifa muhimu, kupata repoti juu ya utendaji wa kampuni na mengine mengi.
Programu hii ambayo inapatikana online kwenye tovuti http://dulaw.co.tz unaweza kuitumia popote ulipo kwa kutumia kifaa chochote, iwe simu au kompyuta ya mpakato. DuLaw tofauti sana na programu nyingine, ambapo yao imetengenezwa mahususi kwa ajili ya mfumo wa Kisheria wa Tanzania, hivyo, hautakiwi kufanya lolote la ziada kuifanya DuLaw iweze kumanage taarifa zako za kisheria kwa matakwa ya hapa Tanzania.
Dudumizi tukiwa moja ya kampuni bora za Website Design hapa Tanzania, tunakuhakikishia usalama na ulizinzi wa bidhaa hii. Dulaw inafanyiwa backeup kila siku huku kila akaunti ikitumia njia bora za kuchunga taarifa za kwenye mitandao.
Gharama ya programu hii ni rahisi zaidi ambapo unaweza kulipia kila mwezi au kwa mwaka, kwa 50,000TZS unaweza kuwa miongoni mwa wanasheria walioboresha utendaji kazi wao kwa kutumia Dulaw. Kwa maelezo zaidi tembelea www.dulaw.co.tz 
Wanafunzi wa Shule ya Sheria Tanzania (law School) wakifuatilia kwa umakini mafundisho ya DuLaw
Mr Nyoni akifafanua thamani ya teknolojia ya habari (IT) kwenye idara ya Sheria Tanzania
Ingawa darasa lilikuwa ni kubwa, ila Wanafunzi wa Sheria katika Shule ya Sheria Tanzania walikuwa wanafuatilia kwa umakini kabisa.
Unaweza kuangalia Online Demo ya programu hii kwa kwenda https://demo.dulaw.co.tz, pia unaweza kupata taarifa zaidi juu ya Dulaw kwenye website yetu http://dulaw.com au tuandikie info at dudumizi.com

No comments :

Post a Comment