Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini
,Constatine Kanyasu,akizungumza na wananchi wa kata ya Buhala hala
wakati aliipokwenda kusikiliza kero ambazo zimekuwa zikiwakabili kwenye
maeneo ambayo wanaishi.
Maeneo ambayo wananchi walibomolewa nyumba zao.
Moja kati ya wananchi ambao wameuzulia Mkutano huo akielezea kero yake kwa Mbunge wa Geita mjini wakati wa Mkutano huo.
Meza kuu ikiongozwa na Mbunge wa
Geita,Mjini,Diwani wa kata ya Buhala hala pamoja na baadhi ya wajumbe
wakifatilia maelezo kutoka kwa wananchi.
Wananchi ambao walikuwa wamejitokeza
kwenye mkutano huo wakisikiliza wakati Diwani wa kata ya Buhala hala
alipokuwa akitoa maelezo na kujibu baadhi ya changamoto za wananchi.
Steven John ambaye ni moja kati ya wananchi ambao wamebomolewa makazi yao akielezea namna ambavyo alivyo bomolewa makazi yake.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji
wa Geita,ambaye pia ni afisa Mipango Luciano Bundala,akijibu kero za
wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa Geita Mjini.
Diwani wa kata ya Buhala hala,Mussa Kabesse akifafanua na kutoa majibu juu ya maswali ambayo yalikuwa yameulizwa na wananchi.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Mbunge wa Geita Mjini Constatine
Kanyasu amesikitishwa kwa kitendo cha wananchi waliokuwa wamejenga
kwenye hifadhi ya misitu kubomolewa huku wengine wakiachwa katika maeneo
hayo na kuahidi kushughulikia ili haki itendeke sawa na wale ambao
hawajabomolewa.
Hayo aliyasema kwenye mkutano wa
hadhara ambao umefanyika kwenye mtaa wa Mwatulole kata ya buhala hala
wilaya na Mkoa wa Geita,wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za
wananchi katika jimbo ambalo analiongoza.
Mh Kanyasu amesema kuwa
amesikitishwa na hatua ya TFS kubomoa nyumba za watu wengine huku wale
wenye uwezo wakiachwa na kuendelea kukaa kwenye maeneo hayo kutokana na
hilo wameagiza watu wa TFS kuangalia kama wale waliobomolewa pale
yalikuwa ni maeneo yao na ninani ambaye aliwauzia.
“Naomba Nikiri na mimi iliniuma
sana lakini kwa sababu ni serikali na sikuwepo na sijui kama walitumia
sheria mimi naomba yeyote ambaye ni haki yake ya msingi alete na mimi
nitashughulikia”Alisema Kanyasu
Hata hivyo Bi,Chausiku Lusetula
ambaye ni miongoni mwa wanananchi waliobomolewa makazi yao amemuomba
Mbunge kuwasaidia ili wapate haki zao za msingi na kwamba kwa sasa
hawana makazi ya kuishi baada ya makazi yao kubomolewa.
“Mheshimiwa Mbunge sisi ni watu
ambao tumekosa makazi kwa sasa hatujui ni wapi tutaishi na
chakusikitisha kwanini sisi tubomolewe na wengine waendelee kukaa kwenye
maeneo ambayo inasemekana ni hifadhi ya misitu kama ni hivyo ni vyema
haki itendeke kwa wote”Alisema Chausiku
Diwani wa kata ya Buhala hala
,Mussa Kabese amewaambia wananchi kuwa mbunge wa jimbo la Geita Mjini
tayari amekwisha mwandikia Waziri mwenye dhamana barua ambayo imemwomba
matumizi ya pori la buhala hala kubadilishwa na kuwekwa taasisi ambazo
zitawasaidia wananchi ambao wapo kwenye mitaa ya shinde na magogo kupata
mahitaji ya msingi ikiwemo swala la elimu na afya.
Hatua hii imekuja ni baada ya
takribani wiki mbili kumalizika ambapo wananchi ambao wamejenga kwenye
hifadhi ya misitu inayosimamiwa na wakala wa misitu nchini TFS
kubomolewa makazi yao.
No comments :
Post a Comment