Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Sightsavers Tanzania Gospert Katunzi akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud
Thabit Kombo mashine ya uchunguzi wa uwoni baada ya kufungua kambi ya
uchunguzi wa macho katika kijiji cha Uroa Mkoa Kusini Unguja. (kushoto)
Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba ambae alifanikisha
kambi hiyo.
Abdulrahaman Abdalla wa Kitengo
cha macho cha Mikunguni akimfanyia uchunguzi wa macho mwanafunzi Hafsa
Suleiman Ali katika kambi ya uchunguzi wa macho Kijiji cha Uroa
inayoendeshwa na Lions Club ya Dar es salam.
Mratibu wa Lions Club ya Dar es
salaam Mustasir Gulamhussein akimuhoji Bibi Saumu Pandu Simai namna
anavyoweza kuona baada ya kumpima na kumpatia miwani kutoakana na
matatizo aliyonayo.
Mbunge wa Jimbo la Chwaka
Bangwanji Mensuria Mshamba akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo
waliofika kufanyiwa uchunguzi wa macho na kupatiwa dawa na miwani kwa
waliobanikia na matatizo ya uwoni.
Baadhi ya wananchi waliofika Skuli ya Uroa kuchunguzwa afya ya macho wakimsikiliza mbunge wao Bangwanji Mensuria Mshamba.
Picha ya pamoja ya viongozi wa
Lions Club ya Dar es salaam, wanaoendesha kambi ya uchunguzi wa macho,
wakiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba
na Waziri Mahmoud Thabit Kombo.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
No comments :
Post a Comment