Friday, February 3, 2017

WABUNGE WANAWAKE WAADHIMISHA MIAKA 40 YA CCM KWA KUFANYA MAZOEZI


ACKSO
Na: Lilian Lundo – MELEZO – Dodoma.
Wabunge Wanawake, wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,    wameadhimisha miaka 40 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya Mazoezi ya Viungo vya Mwili katika Viwanja vya Jamhuri vilivyopo Mjini Dodoma.

Akiongea na Vyombo vya Habari alfajiri ya leo, mara baada ya kumaliza mazoezi hayo, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa wameamua kuadhimisha miaka 40 ya CCM kwa kufanya mazoezi kutokana na mazoezi humpa mtu furaha, upendo pia yanaunganisha watu.
Aliendelea kwa kusema kuwa, kufanya mazoezi kuna punguza  maambukizi ya magonjwa yasiyoambukiza hivyo ni vyema kila mmoja kufanya mazoezi kama ambavyo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inavyosisitiza juu ya watanzania kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa hayo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa imezoeleka katika jamii ya kitanzania kuona wanaume ndio washiriki wakubwa wa michezo na mazoezi lakini ukweli ni kwamba wanawake ndio wanaohitajika kufanya mazoezi zaidi kutokana na kuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa kuliko wanaume.
“Ni wakati wa Watanzania kubadilika na kuwashilikisha watoto wa kiume kufanya kazi za nyumbani ili watoto wa kike nao wapate nafasi ya kushiriki michezo au mazoezi kama ilivyo kwa watoto wa kiume,” alisema Anastazia Wambura.
Nae, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kuwa, mazoezi yamemsaidia awe na afya njema kutokana na kuwa mshiriki mzuri wa kufanya mazoezi kila siku.
Vile vile Mabula amesema kuwa, kufanya mazoezi kumemfanya aonekana kijana zaidi ya umri aliona, hivyo amewataka wanawake kumuunga mkono Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kupanua wigo wa kufanya mazoezi.

No comments :

Post a Comment