Na Immaculate Makilika, MAELEZO, Dar es salaam
Gavana wa Jimbo Katanga Jean
Claude Kazembe amesema kuwa ili urahishaji wa ujenzi wa daraja katika
mto Lwapula uliopo katika mpaka wa Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo(DRC) utasaidia kurahisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya
Dar es salaam kwenda Jimbo la Hault Katanga DRC.
Gavana huyo ametoa kauli hiyo leo
jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya ziara
yake katika Badari ya Dar es salaam.
Alisema kuwa endapo nchi za Zambia
na DRC zitakubaliana kujenga Daraja hilo, kutaimarisha biashara pamoja
na kukuza uchumi wa nchi za Tanzania, DRC na Zambia kwa kuwa itachukua
muda mfupi kwa Wasafirishaji wa Mizigo kutoka Dar es salaam kwenda DRC.
“Kujengwa kwa daraja hilo
kutarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka nchini Tanzania kwenda
nchini DRC, na hivyo kufanya gharama za usafirishaji wa mizigo kupungua”
alisema Gavana Kazembe.
Gavana Kazembe aliongeza kuwa
daraja hilo litakalogharimu dola milioni 85 litakalikuwa na urefu wa
mita 700 linatarajiwa kujengwa kwa ushiririkiano wa Serikali za nchi
za Tanzania, Kongo na Zambia kwa vile litanufaisha nchi hizo kiuchumi.
Aidha, Gavana Kazembe alisema kuwa
atajitahidi kushauri Serikali hizo zijenge daraja katika mto Lwapula
ili kusaidia Bandari ya Dar es salaam kuendelea kutoa huduma nzuri za
usafirishaji wa mizigo kati ya Dar es Salaam na Kongo.
Aidha, alisema kuwa katika
mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa alifurahishwa na hatua hiyo kwa kuwa itasaidia kukuza urafiki
uliopo baina ya Tanzania na Kongo pamoja na kurahisisha usafirishaji wa
mizigo na kwa gharama nafuu.
No comments :
Post a Comment