Makamu wa Rais wa TCCIA Viwanda Octavian Mshiu akibadilishana nyaraka na Rais wa Chamber ya Biashara ya Uturuki
Chemba
ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) inatajia kufanya ziara ya
Kibiashara Nchini Italy na Uturuki mapema mwezi Mei 2017.Akizungumza na
waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Ndugu Gotfrid
Muganda alisema “ Lengo kubwa la ziara hii ni kuwawezesha wafanya
biashara wa Tanzania kutanua wigo wa masoko na fursa za kibiashara na
kubadilishana ujuzi“. Pia tukiwa Uturuki tunatazamia kusaini mkataba wa
ushirikiano na chemba ya biashara ya Uturuki hii inafuatia ziara ya Rais
wa Uturuki Nchini Tanzania.
kizungumza
juu ya ziara hiyo Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa Biashara
na Masoko wa TCCIA Imani Kajula alisema “ Ukuzaji wa masoko ya nje ni
mkakati endelevu ambao sio tu utaongeza soko nje lakini pia kuleta urari
mzuri wa biashara na hivyo kusaidia kuimarisha pia thamani ya
shilingi”. Aliwaambia wafanya biashara ambao ni wanachama na wasio
wanachama wanakaribishwa kujiandikisha kuanzia sasa hadi tarehe 3 March
2017. Kwa taarifa zaidi info@eagroup.co.tz au muganda@tccia.com


No comments :
Post a Comment