Meneja Uboreshaji wa Uzalishaji wa TBL,Charles Nkondola
Wafanyakazi wa TBL Group wamekuwa wakishiriki kampeni mbalimbali za mazingira na kupanda miti
Moja ya Paneli ya kisasa ya umeme wa nishati ya jua katika kiwanda cha TBL Mbeya
Wafanyakazi
wa kiwanda cha TBL cha Mwanza wakimimina pumba za mpunga kwenye mtambo
unaotumia nishati mbadala zisizo na athari kwa mazingira katika
uzalishaji
…………………………………………………………………………
–Kushirikiana na serikali na wadau wengine kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji
-Tayari imeanza kutumia teknolojia zisizochafua hewa wakati wa uzalishaji na kupunguza matumizi ya maji katika uzalishaji
Kampuni
ya TBL Group imeeleza mkakati wake wa kuendelea kutekeleza malengo ya
dunia kuhusiana na kutunza mazingira hususani katika maeneo ya kulinda
vyanzo vya maji,nishati,uzalishaji unaochafua hewa ,udhibiti na utunzaji
taka.Mkakati huu unaenda sambamba na utekelezaji wa moja ya sera ya
kampuni ya “Kujenga Dunia Maridhawa” (Better World).
Baadhi ya hatua za kulinda mazingira ambazo kampuni inaendelea kuzitekeleza ni kutumia
teknolojia zisizochafua hewa wakati wa uzalishaji katika viwanda
vyake,kushiriki kampeni za kupanda miti na utunzaji wa vyanzo vya
maji,kushiriki kampeni za matumizi ya maji kwa umakini,utakatishaji wa
maji taka na kuharibu taka ngumu na nyepesi kwa kutumia teknolojia za
kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.
Hivi
sasa kampuni inalipa kipaumbele zaidi suala la kushirikiana na
serikali, wadau mbalimbali na wananchi kuhakikisha inakabiliana na
changamoto ya upungufu wa maji ambayo inatishia kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchini na sehemu nyinginezo duniani.
Meneja
Uboreshaji na Uzalishaji wa TBL Group,Charles Nkondola, amesema mkakati
huu shirikishi wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji ni wa kudumu na uko kwenye sera ya kampuni kwa kuwa moja ya malighafi kubwa katika uzalishaji wa bidhaa zake ni maji.
“Moja ya sera ya kampuni yetu ni “Kujenga
Dunia Maridhawa” (Better World) ambayo inalenga suala la kulinda
mazingira na vyanzo vya maji ,matumizi mazuri ya maji na nishati kwa
ajili ya kuepusha madhara mbalimbali kama vile ukame ambao unasababisha
upungufu wa chakula na matatizo mengine ya kiafya.Matumizi yetu ya maji
tumeyapunguza kutoka hectolita 6 za maji katika miaka ya karibuni hadi
hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa”.Alisema Nkondola.
Bw.Nkondola alisema TBL Group inaliangalia suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji sio kwa kiwango cha maslahi ya viwanda vyake kupata malighafi tu bali kwa jamii nzima ambapo kampuni inafanyia biashara kwa kuwa sera ya kujenga Dunia Maridhawa inashahabiana Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) na suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni moja ya suala ambalo limepewa umuhimu mkubwa.
Alisema kutokana na dalili za mabadiliko ya hali ya hewa zinazoendelea kujitokeza duniani hivi sasa kuna umuhimu mkubwa wa kutekeleza kwa vitendo maazimio yaliyofikiwa na wakuu wa nchi mbalimbali katika mkutano wa Mazingira uliofanyika mjini Paris,nchini Ufaransa mwaka
juzi,ambapo kuhusiana na hali ya hewa moja ya ajenda ilikuwa kuangalia
uwezekano wa viwanda kufanya uzalishaji usioathiri mazingira.
Katika
utekelezaji wa ajenda hii,Nkondola,alisema TBL Group inaendelea kufanya
uwekezaji kwenye matumizi ya teknolojia za kisasa za kufanya uzalishaji
bila kuathiri mazingira na tayari imeanza kufanya
uzalishaji kwa kutumia umeme unaotokana na nishati ya jua katika
kiwanda chake kilichopo mkoani Mbeya na teknolojia ya kufanya uzalishaji
kwa kutumia pumba za mpunga katika kiwanda cha Mwanza.
Alisema
matarajio ya matumizi ya teknolojia ya umeme ni kupunguza tani 130 za
hewa chafu (Carbon Emmision) kwa mwaka na kampuni inao mkakati
kuhakikisha teknolojia hii inasambazwa katika viwanda vyake vyote vilivyopo nchini na alitoa ushauri kwa viwanda vingine vilivyopo nchini kuangalia uwezekano wa kufanya uzalishaji kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.
Alitoa
wito kwa watanzania wote kuzingatia suala la utunzaji wa mazingira
hususani kupanda miti ,kulinda vyanzo vya maji na kutumia maji kwa
umakini.
No comments :
Post a Comment