Tamko
la chama cha kutetea haki za wanaume Tanzania kuhusiana na tukio la
mauaji yaliyofanywa na Mohamed Mohamed mkazi wa Boko Jijini Dar es
salaam tukio ambalo limeteka hisia za wengi kuwa mwanaume huyo ametenda
kosa bila kuangalia pande zote ili kujua chanzo cha tatizo la wanandoa
hao.
Chama
cha kutetea haki za wanaume Tanzania TAMRA kimepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa ya mauaji yaliyotokea huko Boko Dar es salaam kutokana
na hatua zilizochukuliwa na mmoja wa wanaume aitwaye Mohamed Mohamed
(46) mfanyabiashara mkazi wa boko jijini dar es salaam kwa kumuua mkewe
sophia(36) na kisha yeye mwenyewe kujiua na kuacha ujumbe kurasa 80
ujumbe ambao kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi ndiyo umebeba
sababu mauaji hayo.
Kimsingi,jamii
imekwenda mbali katika tukio hili kwa kuwachukulia wanaume kuwa ni
wabaya,ni katili, sawa lakini chama hiki kinaomba jamii itambue uwepo wa
migogoro mikubwa inayofukuta ndani ya ndoa zetu huku chanzo kikubwa
kikiwa ni baadhi ya akina mama,nasema hivyo kutokana na ushahidi
kwamba,tafiti zilizofanyika hapo nyuma zilionyesha kuwa katika mikoa
minne ikiwemo lindi Mtwara, Dar es salaam na Zanzibar ilionyesha kuwa
wanawake walikuwa wakiongoza kwa kupiga wanaume ikiwamo kuwanyima
unyumba huku wanaume wakikosa pa kusemea kutokana na kutokuwepo kwa
chombo hiki mpaka pale chama hiki kilipoanzishwa .
Matatizo
mengine ukiachilia kupigwa wanaume wamekuwa wakipambana na vituko vingi
ikiwemo ukatili wa kijinsia kwa kutengwa na familia wakiwemo watoto
kuambatana na misimamo ya mama huku baba akibaki mkiwa na baadaye
kupelekea vifo vingi kwa akina baba.
Tafiti
zinaonyesha kuwa wanaoathirika zaidi ni wanaume hasa waliostaafu kazi
serikalini taasisi na mashirika kwamba wanapokuwa wamekoma kupata fedha
kwa ajiri ya kutunza familia hutengwa na baada ya muda huugua magonjwa
makubwa ikiwemo kupooza,sukari,nk.
Yote
haya yanatokana na mwanaume kushindwa kuthaminiwa utu wake na
kudharauliwa na familia na hapo ndipo hujikuta katika lindi la mawazo na
kupelekea kupoteza maisha.
Katibu
mkuu wa chama cha kutetea haki za wanaume Antony Sollo amejaribu
kufuatilia suala hili kuona jamii imelipokeaje tukio hili ambapo watu
mbali mbali wameweza kuelezea hisia zao.
Akizungumza
na katibu mkuu wa TAMRA Seif Hemed mkazi wa Uhuru jijini Mwanza ametoa
maoni yake kuhusiana na tukio hilo na kusema kwamba tukio hili
limesababishwa na mwanamke kutokana na majibu aliyokuwa akimjibu
mwanandoa mwenzake hususani pale alipotamka kwamba watoto waliozaa si
wake,matumizi mabaya ya fedha za mmewe jambo ambalo linaumiza moyo.
“Hata
kama ningekuwa mimi nisingeweza kuvumilia kwa kuwa mke nimeshiriki
kumtafuta kumlipia mahari,kumtunza kwa kumpatia mahitaji mbalimbali
ikiwemo kulea ujauzito na kuwalea watoto nikijua ni mali yangu halafu
leo mtu anaibuka na kusema kuwa watoto hawa si wangu inauma sana”,
alisema Seif.
Kufuatia
hali hii TAMRA haina ugomvi na wanawake ila inawataka wanandoa
kuheshimu ndoa kwani ni agizo la mungu kwamba enendeni mkazaliane
muijaze dunia ambapo baada ya agizo hilo muungu aliagiza mambo mawili
ikiwemo wajibu wa kila mwanandoa.
Wwapo
wanandoa watamheshimu mungu na kutekeleza wajibu wao kila mmoja ndoa
hizo zitadumu na amani ndani ya ndoa hizo itakuwa ni ya milele.
Haya ni Maagizo ya mungu kwa wanandoa.
Kwa wanawake :
WAEFESO 5 : 22 neno la Mungu linasema enyi wake watiini waume zenu kama
kumtii Bwana wetu , kwa maana Mume ni kichwa cha Mkewe,kama kristo naye
ni kichwa cha kanisa naye ni mwokozi wa mwili lakini kama vile kanisa
limtiivyo kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila
jambo.
Kwa Wanaume: Waefeso 5: 25 Enyi
waume wapendeni wake zenu kama kristo naye alivyolipenda Kanisa
akajitoa kwa ajiri yake,ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji
katika neno apate kujiletea kanisa tukufu lisilo na ila wala kunyanzi
wala lolote kama hayobali liwe takatifu lisilo na mawaa vivyo hivyo
imewapasa waume zao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe ampendaye
mkewe hujipenda mwenyewe,hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote bali
huulisha na kuutunza kama kristo naye alivyolitendea kanisa.
Hivyo nachukua nafasi hii kuiomba jamii mambo yafuatayo:
1. Kuheshimu neno la Mungu ili kuweza kudumisha ndoa zetu.
2. Kuwa wavumilivu katika shida na raha kama viapo tulivyoapa mbele za Mungu
3. Tuweze
kujifunza masomo ya ndoa ili kuingia katika ndoa tukiwa na ujuzi juu ya
wajibu wetu baada ya kuingia katika Tasnia hii muhimu ya ndoa.
4. Tumtegemee
Mungu katika mambo yote na tukio hili liwe fundisho kwetu tujipeleleze
ni wapi tuna Mgogoro usioisha katika ndoa zetu ili kuepuka Mauaji ya
aina hii.
IMEANDALIWA NA:
Antony Johnson Sollo
KATIBU MKUU TAMRA TANZANIA
1. 0767 203 556 BERENS CHINA Mwenyekiti TAMRA
2. 0762 117 117 ANTONY JOHNSON SOLLO Katibu Mkuu TAMRA
No comments :
Post a Comment