Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea
kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali
ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi
na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na
wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa
matukio makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima
dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio
yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-
KUKAMATA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UUZAJI/USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.
Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa
02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika
maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha
na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji
na watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha
ba usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1. SHABAN RAMADHAN
[40] Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35] Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA
[60] Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN [22] Mkazi wa Airport –
Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde.
Watuhumiwa wote wapo mahabusu na
mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu
wanaojihusisha na dawa za kulevya.
KUKAMATA WAUZAJI/WASAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.
Aidha kufuatia misako iliyofanyika
kuanzia tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo
mbalimbali Mkoani Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio
mawili tofauti wakiwa na dawa za kulevya.
Katika msako wa kwanza uliofanyika
maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na
Mkazi wa Ilemi alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa za kulevya aina ya
Heroine.
Pia katika msako uliofanyika maeneo ya
Mbalizi, ANITHA ABEL [21] Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika shule ya
Sekondari Sanani iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na Mkazi wa
Mbalizi alikamatwa akiwa na kete 15 za dawa za kulevya aina ya Heroine
akiwa nyumbani kwao.
Mtuhumiwa anaishi na mama yake mzazi
aliyefahamika kwa jina la MARTHA MWALINDU ambaye alikimbia baada ya
kuwaona askari na inasadikika ndiye muuzaji/msambazaji mkubwa wa dawa
hizo za kulevya na huwa anamtumia mtoto wake kuuza na kusambaza. Msako
mkali wa kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya Upelelezi kukamilika.
KUKAMATA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA [MATEJA].
Aidha katika misako mbalimbali
iliyofanyika walikamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na utumiaji wa dawa
za kulevya maarufu kama Mateja ambao ni:-
- AYUBU ABDALLAH [42] Mkazi wa Ilomba jijini Mbeya
- EMANUEL SIMBEI [43] Mkazi wa Sokomatola
- IMAN ABBAS [33] Mkazi wa Majengo
- SHABAN SHAIBU [19] Mkazi wa Nonde
- KENY SANGA Mkazi wa Sokomatola
- PASCHAL PIUS [28] Mkazi wa Itiji
- PILIM KAYANGE [20] Mkazi wa Uhindini
- ELISHA MWAIHABI [19] Mkazi wa Nonde
Wengine ni:-
- DANIEL KANJANJA [43] Mkazi wa Uhindini
- MUSSA KIPESA [37] Mkazi wa Iwambi
- CHARLES GERVAS [28] Mkazi wa Nonde
- KIMANZI KILONZA [44] Mama John
- SHABAN SHAIBU [26] Mkazi wa Nonde
- EMANUEL LUCAS [18] Mkazi wa Ilomba
- RICHARD GONDWE [40] Mkazi wa Ivumwe
- HENRY LEMA [35] Mkazi wa Mama John
- RAMADHAN ABBAS [18] Mkazi wa Sae
- EDWARD MWASEKA [30] Mkazi wa Majengo
- LUSEKELO KIDION [26] Mkazi wa Mwakibete
- ALINANUSWE STIVEN [26] Mkazi wa Ilolo
- JUSTIN WISTON [23] Mkazi wa Mafiati
- MICHAEL KASHILILIKA [20] Mkazi wa Manga
- KANI ASANGALWISYE [28] Mkazi wa Ituha.
Watuhumiwa wapo mahabusu wanaendelea kuhojiwa ili kupata mtandao halisi wa wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.
KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI].
Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa
02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako dhidi ya
watu wanaojihusisha na uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Katika
misako hiyo iliyofanyika maeneo ya Mabatini na Ilomba jijini Mbeya,
watuhumiwa wanne walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi
misokoto mitatu yenye uzito wa gram 15.
Watuhumiwa waliokamatwa ni 1. GEOFREY
ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini 2. ZUBER MWAMBENYA [24] 3. GWAKISA
ANYOSISYE [20] wote wakazi wa Mama John na 4. PHILIBERT MOSES [35] Mkazi
wa Nonde.
KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya
kuanzia saa 17:00 hadi saa 17:45 jioni msako ulifanyika maeneo ya Soweto
Mtaa wa Mkombozi, Kata ya Ruanda na maeneo ya Nonde, Kata ya Nonde,
Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kuwakamata
watuhumiwa wawili wakiwa na miche ya Bhangi 18 na mbegu zake.
Watuhumiwa hao ni 1. DENIS DAVID [30]
Mkazi wa Soweto ambaye alikamatwa akiwa dukani kwake na 2. STIVIN
VENANCE [18] Mkazi wa Nonde. Upelelezi unaendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linaendelea na mahojiano na watuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa
watu wanaojihusisha nao katika biashara ya dawa za kulevya.
KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO]
Mnamo tarehe 10.02.2017 majira ya saa
21:00 usiku katika msako uliofanyika huko maeneo ya Mafiati, Kata ya
Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya watuhumiwa wawili
walikamatwa wakiwa na Pombe Moshi ujazo wa lita 10.
Watuhumiwa hao ni 1. FRANCIS NDEZI
[32] Mkazi wa Forest na 2. JAMES KAJANJA [38] Mkazi wa Forest ya Zamani.
Upelelezi unaendelea.
KUKAMATA WATUHUMIWA WANAJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA NA KUTEKA MAGARI.
Mnamo tarehe 12.02.2017 kuanzia majira
ya saa 20:00 hadi saa 23:45 Usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
lilifanya msako huko katika vijjiji vya Mabadaga na Mpakani vilivyopo
Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya jirani na barabara kuu ya Mbeya kwenda
Njombe. Msako huo ulilenga kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na matukio
ya unyang’anyi wa kutumia na silaha na utekaji magari wakati wa usiku.
Katika msako huo jumla ya watuhumiwa
11 wamekamatwa ambao ni 1. EMANUEL MANGA [30] Mkazi wa Njombe 2. ZAWADI
MAKOGA [33] Mkazi wa Makambako 3. ISSA ABIBU [45] Mkazi wa Mbeya 4.
FRICK MCHAMI [26] Mkazi wa Machimbo 5. MPAJI KAPUNGU [38] Mkazi wa
Lugelele na 6. RICH KIHOMBO [25] Mkazi wa Ubaruku.
Wengine waliokamatwa ni 7. MUSSA
MTWEVE [27] Mkazi wa Machimbo – Mbarali 8. WILBERT MAGAINA [36] Mkazi wa
Mlomboji 9. IBRAHIMU TWEVE [35] Mkazi wa Mlomboji – Mbarali 10. JOHN
MBAFO [48] Mkazi wa Machimbo na 11. ZABRON MWILONGO [20].
Aidha katika msako huo Pikipiki 4
zilikamatwa baada ya watuhumiwa kuwaona Polisi na kuzitelekeza na
kukimbia. Pikipiki hizo ni yenye namba 1. MC 254 BHK aina ya Kinglion 2.
MC 264 AZZ aina ya Kinglion 3. MC 521 BYC aina ya Sanlg na 4. MC 565
BGE aina ya Kinglion. Upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa
watu wanaojihusisha na matukio hayo.
KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU.
Mnamo tarehe 13.02.2017 majira ya saa
09:00 asubuhi huko Eneo na Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na
Mkoa wa Mbeya, wahamiaji haramu watatu wote raia na wakazi wa nchini
Ethiopia walikamatwa kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Wahamiaji hao ni 1. AGAFA SHAMENO [22] 2. BEKELE SEDESO [29] na 3. SESEBE SHIFUHA [24]. Upelelezi unaendelea.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu
Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi
kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu na mtandao wa watu
wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ili wakamatwe na hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yao. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito
kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara haramu ya
dawa za kulevya kwani inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na
kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments :
Post a Comment