Mbunge wa jimbo la
Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa akimpongeza aliyekuwa meneja wa kampeni za
chama cha mapinduzi(CCM)kitongoji cha Magomeni B kata ya Nianjema,alhaj
Abdul Zahoro kwa ushindi alioupata,Rajabu Swedy na kuibuka na kura 441
dhidi ya vyama vya upinzani.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa kata ya Magomeni
Mwanaharusi Jarhuf(kushoto),na diwani wa kata ya Nianjema Abdul
Pialla9kulia) wakimwinua mkono mwenyekiti mteule wa kitongoji cha
Magomeni B Rajabu Swedy baada ya kutangazwa mshindi .(Picha na Mwamvua
Mwinyi)
……………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MWENYEKITI mteule wa kitongoji
cha Magomeni B, Nianjema, Bagamoyo,kupitia CCM, Rajabu Swedy
amewashukuru wananchi wa kitongoji hicho kwa kumchagua kuwa mwenyekiti
wa kitongoji hicho.
Aidha amesema amejipanga kuleta maendeleo na kusimamia kero ya miundombinu ya
barabara, maji na umeme.
Swedy ameeleza kwamba hana chuki kwa wale ambao hawakumpigia kura kwani inaonyesha kukua kwa demokrasia .
Aliyasema hayo baada ya kutangazwa kuwa mshindi dhidi ya vyama vingine vitatu vya upinzani.
Alimpongeza mwenyekiti wa
jumuiya ya wazazi wilayani humo, alhaj Abdul Sharif kwa kumsimamia
kwenye kampeni zake,mbunge, na viongozi wengine wa chama kwa kuhakikisha
ushindi unapatikana.
Swedy alieleza kuwa kampeni na
uchaguzi umeisha kilichobakia kwasasa ni kuchapakazi na kuwatumikia
wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa.
“Nawashukuru wananchi wote
walionipigia kura mimi,natambua wengine sio wananchama wa CCM lakini ni
kuguswa kwao kwa namna chama tawala kinavyotekeleza ilani yake”
“Na wahakikishia nitashirikiana
na kila mmoja na nitawahudumia wananchi wote bila ya kuwabagua kwa
kuleta maendeleo kwenye kitongoji hiki,” alisema Swedy .
Swedy akizungumzia wagombea wa
vyama pinzani kushindwa kupewa ridhaa, alisema isiwe sababu ya kuwagawa
wananchi ama kumbeza mshindi kwani huo unakuwa sio ukomavu wa kisiasa.
“Nitashirikiana nao katika suala la maendeleo ili kuhakikisha kitongoji kinapiga hatua kimaendeleo,” alisisitiza Swedy .
Alisema wananchi wasiwe na wasi
wasi kwani kukichagua Chama Cha Mapinduzi ni kuchagua maendeleo hivyo
wasubiri kuona utekelezaji kwa kushirikiana na chama,
serikali,halmashauri pamoja na wadau. .
Swedy anasema kipaombele chake
kikubwa ni kufungua njia mbalimbali zilizokuwa hazitumiki ili
kuwarahisishia wakazi wa kitongoji hicho waweze kupita.
Aliyekuwa meneja wa kampeni
katika kitongoji hicho, alhaj Abdul Sharif alishukuru wananchi kwa
kumuamini na kukiamini chama kumsimamisha kupeperusha bendera ya CCM.
Alhaj Sharif alieleza, siasa za majukwaani zimemalizika, kikubwa ni kuwa na subira kungojea utekelezaji wa yale yaliyoahidiwa.
Awali msimamizi msaidizi wa
uchaguzi kata ya Nianjema, Cezary Madasha, alimtangaza Swedy (CCM) kuwa
mshindi kwa kupata kura 441 .
Huku Furaha Salehe wa(CHADEMA)akiwa na kura 332 ,Jumaa Chambo (CUF) kura 140 na Wema Abdullah (ADC) kura sita.
No comments :
Post a Comment