Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen amekutana na wadhibiti ubora wa shule wa
halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa kujua changamoto wanazokumbana nazo na
mambo yanayopelekea kushuka kwa elimu katika mkoa wa Rukwa.
Zelote Stephen alifikia uamuzi wa
kuwaita wadhibiti hao baada ya Mkoa wa Rukwa kushuka kielimu kutoka
nafasi ya 6 mwaka 2015 hadi nafasi ya 12 kati ya Mikoa 31 kwa mwaka 2016
kwa mitihani ya kidato cha 4, na pia kuteremka katika mitihani ya
kidato cha pili kutoka
nafasi ya 20 kwa mwaka 2015 hadi nafasi ya 21 kwa
mwaka 2016.
Wadhibiti hao walielezea sababu
kede kede zilizopelekea kushuka kwa kiwango cha elimu katika Mkoa wa
Rukwa na miongoni mwao ni kutopewa mrejesho wa taarifa za kila wiki
wanazoziandika na kukabidhi kwa wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa
wilaya.
“Toka Mwezi July mwaka jana
tumeshaandika ripoti nyingi tu zinazoelezea mapungufu kama vile,
upungufu wa waalimu kwa baadhi ya masomo, matundu cha vyoo, vitabu vya
kusomea, nakadhalika lakini hakuna hata mrejesho tunaoupata kutoka kwa
Mkurugenzi,” Goreth Ntulo alieleza.
Kwa upande mwingine sababu
zinazokwamisha ufanisi wa kazi za wadhibiti hao wanadai kutopewa motisha
na mwajiri wao na kuwasababisha kuishi katika maisha magumu.
“Mimi sijawahi kwenda likizo kwa
fedha ya serikali tangu nianze kufanya kazi na madarasha hatupandishwi n
ahata ukipandishwa inabaki jina tu lakini mshahara upo pale pale na
kuapata hiyo fedha ya daraja ulilopandishwa ni kazi kubwa ya kukatisha
tamaa,” Mmoja wa wadhibiti hao Mama Jairo alifafanua.
Nae Mkuu wa Mkoa baada ya
kusikiliza malalamiko hayo aliwaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha
kwamba wadhibiti hao wanapatiwa mrejesho juu ya kasoro walizozibaini
baada ya kufanya ukaguzi katika mashule hayo.
“Kwani hizi shule ni za nani?, Si
ni za wakurugenzi, sasa naagiza wakurugenzi wote wawe wanatoa mrejesho
kwenu ili muweze kujua ni lipi linawezekana kurekebishika na kwa kipindi
gani na nili lipi haliwezekani ili Mkae mkijua, bila ya hivyo itakuwa
haina maana nyinyi kufanya ukaguzi halafu ripoti zikarundikwa kwenye
madroo,” Zelote Stephen alikazia.
Pia Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza
wakati wakaguzi hao wanawapa wakurugenzi ripoti hizo wahakikishe kuwa
wanawapa na “dead line” na wakurugeni wazingatie na wawaheshimu na
kuwathamini ili kila mmoja afanye kazi yake ambayo ameajiriwa nayo.
“Kama Mlikuwa na uwoga muondoe
ofisi hii itawapa sapote, na make mkijua kuwa tunawathamini sana maana
kupitia nyinyi tunajifunza mengi sana ambayo ndio yanatupa mpango
mkakati wa kuhakikisha tunapeleka elimu mbele,” Zelote Stephen
aliwahakikishia.
Mmoja wa wadhibiti hao Pracida
Rwegasira alitoa shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa
kuchukua uamuzi wa kuwaita ili kutoa mchango wao katika kupeleka sekta
ya elimu mbele na kuongeza kuwa tokea aanze kazi hiyo hawajawahi kuitwa
na Mkuu wa Mkoa.
Nae Katibu Tawala wa Mkoa Tixon
Nzunda aliahidi kutetea haki zao za kiutumishi na kuwa sauti ya kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elmu.
Imeandikwa na
Abdulrahman Salim
Kaimu Afisa habari Mkoa wa Rukwa
No comments :
Post a Comment