Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo
vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la
Utangazaji la Taifa Dkt. Ayub Riyoba akitoa hoja kuhusu umuhimu wa Redio
katika kuunganisha jamii ya watanzania katika maadhimisho ya Siku ya
Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini
Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO
Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues akitoa neno la kwa Serikali na wadau wa
Redio na vyombo vya habari nchini katika maadhimisho ya Siku ya Redio
Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Utangazaji Kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Fredirick Ntobi akifafanua
jambo kwa wadau wa Redio Redio kuhusu Redio za jamii katika maadhimisho
ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO
Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho
ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Mwakilishi
Mkaazi wa UNESCO Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues wakati wa maadhimisho
ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea risala kutoka kwa Mwakilishi
wa Redio za Jamii nchini Bw. Baraka David wakati wa maadhimisho ya Siku
ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na
Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues na
wawakilishi wa vyombo vya habari nchini hususani Redio mara baada ya
kumalizika kwa
maadhimisho ya Siku ya Radio Duniani yaliyofanyika katika
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
……………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri waandishi wa habari nchini
kuwa na utaratibu na desturi ya kusoma na kuelewa Sheria mbalimbali
zinazoendesha tasnia ya Habari nchini.
Ameyasema hayo wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu
huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa usomaji wa Taratibu na Sheria
utasaidia kuondoa mikanganyiko inayojitokeza mara kwa mara kuhusu mambo
mbalimbali.
“Nadhani wanahabari wanapaswa
kuwa na maswali mengi katika jambo unaloambiwa husiamini kila kitu
unachoambiwa pata muda wa kusoma na kujiridhisha”Alisistiza Mhe. Nnauye.
Ameongeza kuwa kila mwanahabari
nchini ana jukumu la kuzisoma kwa kina na kuzielewa Taratibu na Sheria
zinazoendesha tasnia ya habari nchini na kama kuna Sheria yoyote ina
mapungufu basi yawasilishwe kwake na kujadiliwa ili yafanyiwe
marekebisho.
Aidha Mkurugenzi wa Utangazaji
Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Fredirick Ntobi
awaomba wadau wa habari nchini kuendelea kutoa ushirikiano kwao katika
kuendeleza jitihada za kuifanya sekta ya habari nchini kuendelea kuwa
mubimu katika maendeleo ya taifa.
“Niwaombe wadau wa habari nchini
tuendelee kushirikiana kwa dhati katika hili tusome Taratibu na Sheria
zilizopo na kuendelea kutoa maoni yetu pale ambapo kuna mapungufu ili
tuboreshe na kuiendelezaTasnia hii ya habari” Alisisitiza Bw. Ntobi.
No comments :
Post a Comment