Bohari ya Dawa (MSD) hii leo
imekabidhiwa mashine za kupandishia mizigo juu na kushusha (Forklifts)
sita, zenye gharama ya shilingi za Kitanzania Milion 531. 8, ambazo
zimetolewa msaada na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kupitia Shirika
la Marekani la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID).
Msaada huo ni sehemu ya awamu ya
pili ya maboresho ya maeneo ya kuhifadhia dawa ya MSD ualiyokuwa
yakifanywa na Global Fund, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa maghala ya
kisasa
yaani WiB ya MSD Makao makuu, Dodoma na Mbeya, na ujenzi wa
maghala ya Kisasa MSD kanda ya Tabora na Kituo cha mauzo Tanga.
Wakizungumza katika makabidhiano
hayo, katika utekelezaji wa awamu ya mwisho ya upanuzi na ujenzi wa
maghala ya kisasa yanayojulikana kama Warehouse in -a –box, mashine hizo
(forklifts), Naibu Mkurugenzi Mkazi wa JSI/SCMS Marasi Mwencha amesema
fedha hizo ni zile zilizosalia kutoka kwenye ujenzi wa maghala ya
kisasa ya MSD, ambapo walikubaliana na menejimenti ya MSD kununulia
forklift.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amewashukuru wahisani hao kwa mashine hizo ambazo ni za gharama, na kueleza kuwa mashine hizo zitapelekwa kwenye kanda za MSD zenye uhitaji. Hata hivyo ameeleza kuwa tayari MSD ina Kiwanja maeneo ya Luguruni, wilayani Ubungo jijini DSM, kwa ajili ya kujenga ofisi na ghala la kisasa kwa Kanda ya DSM hivyo wanategemea kuendelea kushirikiana na wahisani kwa ajili ya ujenzi pindi taratibu zitakapokamilika.

No comments :
Post a Comment