Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la
Ileje, mkoani Songwe Janeth Mbene, wakati Mbunge huyo alipomtembelea
ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala
mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo lake la Ileje.
Mbunge wa Jimbo la Ileje mkoani
Songwe, Janeth Mbene (kushoto) akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati Mbunge huyo
alipomtembelea Naibu Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam
leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo
lake la Ileje.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Ileje mkoani Songwe, Janeth Mbene, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo lake la Ileje. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment