Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na
wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa
Tathminiya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo) )
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na
wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa
Tathminiya Athari za Mazingira jijini Dar es Salaam jana (leo) ).
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mwandisi Bonaventure Baya akiongea na
wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa
Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo)
Mjumbe wa Bodi wa Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Ruben Mwamakimbullah akitoa
salamu za Bodi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mazingira Prof. Salome
Misana katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam waTathmini ya
Athari za Mazingira Dar es Salaam jana (leo))
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiwa katika
picha ya pamoja na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa
Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es
Salaam jana (leo).(Pichazotena Benjamin Sawe)
………………..
Na: Frank Shija – MAELEZO
Wataalamu wa Tathmini ya Athari za
Mazingira nchini wametahadharishwa kuwepo kwa matapeli wanaingilia
taaluma hiyo kwa lengo la kufanya udanganyifu na kujipatia kipato.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba
wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa
Tathmini ya Athari za Mazingira Tanzania (TEEA) leo Jijini Dar es
Saalam.
Makamba amesema kuwa taaluma ya
tathmini ya Athari za Mazingira ni ya shughuli ambayo inahitaji mkubwa
sana na ni kwa mujibu wa sheria za nchi lakini kumekuwapo na makanjanja
ambao wamekuwa wakifanya uraghai kwa wawekezaji na kutia doa tasnia
nzima ya taaluma ya uthamini wa athari za mazingira.
“Serikali inakusudia kubadilisha
kanuni na taratibu ili kuongeza udhibiti wa udanganyifu katika eneo la
Tathmini ya Athari za Mazingira(IAE) kwa kuweka viwango stahiki kwa
wataalamu wa tathmini ya athari za mazingira vitakavyozingatia elimu na
uzoefu,” alisema Makamba.
Aliongeza kuwa ni vyema sasa
Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na
Chama cha Wataalumu hao kushirikiana kuhakikisha taaluma hiyo
haingiliwi na makanjanja ili kufanikisha utoaji wa huduma zenye viwango
stahiki na vya kuridhisha.
Awali akiwasilisha salamu za Bodi
ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Profesa Ruben
Mwamakimbullah amesema amemshukuru Waziri Makamba kwa kukubali kujumuika
na wataalamu hao katika mkutano huo muhimu na kuongeza kuwa wao kama
Bodi watafanyia kazi ushauri wote alioutoa na kuahidi kuongeza ufanisi
katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta heshi kwa tasnia ya tathmini
ya athari za mazingira na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Bonaventure
Baya amesema kuwa mkutano huo umekuwa ukiwakutanisha Wataalamu wa
Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ambapo utumia fursa hiyo
kukumbushana mambo yanayohusu weledi na majukumu yao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa
mkutano huo ni wa tatu kufanyika ambapo umetanguliwa na mikutano
iliyofanyika februari 2011 na Machi 2015 na kuongeza kuwa NEMC imekuwa
ikiratibu mkutano huo kwa lengo la kuwakutanisha Wataalamu wa Tathmini
ya Athari za Mazingira nchini ili kujadili changamoto zao na kupeana
uzoefu.
No comments :
Post a Comment