Leo Jumamosi Februari 11,2017 kumefanyika kongamano kubwa la Maalum la Maombi kwa Wanavyuo mkoani Shinyanga.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi
wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi katika manispaa ya
Shinyanga na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali mkoani
Shinyanga,viongozi wa vyuo na dini,wanakwaya,wanafunzi wa shule za
sekondari na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Kongamano hilo ambalo ni la kwanza
kufanyika mkoani Shinyanga limetokea baada ya Mtumishi wa Mungu
Happiness Mwaja Kihama kutamani kuwepo kwa kongamano ndipo wanafunzi kwa
pamoja wakakubali kuunganisha nguvu hatimaye kufanikisha kufanyika kwa
kongamano hilo.
Miongoni mwa malengo ya Kongamano hilo
lenye kauli mbiu ya “Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa –Mithali 1:7”ni
kuwaleta pamoja wanafunzi na kuwafanya wafahamiane,kuunganisha nguvu
katika kumuomba mungu kwa ajili ya kuendelea ustawi wa kielimu katika
mkoa wa Shinyanga.
Pamoja na kuuombea mkoa wa Shinyanga
kielimu,kongamano hilo pia lililenga kuwaombea wanafunzi ili mungu
awasaidie kufanya vizuri katika masomo yao sambamba na kuwajengea uwezo
vijana uwezo wa kumjua mungu na kusababisha hofu ya mungu ndani yao ili
kuisadia serikali katika kupunguza vitendo viovu katika jamii.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametusogezea picha 50 za matukio yaliyojiri Mwanzo mpaka Mwisho..Shuhudia hapa chini
Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali mkoani
Shinyanga ikiweo Shycom,Mocu ,wakiwa ukumbini wakati wa kongamano Maalum
la Maombi kwa wanavyuo
Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza
wakati wa Kongamano hilo ambapo alisema ni mara ya kwanza kufanyika
mkoani Shinyanga.Mchungaji Mosha aliwasisitiza vijana hao kumtanguliza
Mungu katika maisha yao
Shija Simon akisoma risala ambapo
alisema wameamua kukutana pamoja ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika
kumuomba mungu kwani wanaamini kuwa maomi hayo yatasababisha mabadiliko
ya kielimu mkoani Shinyanga kwani ukilinganisha na mikoa mingine mkoa wa
Shinyanga bado upo chini kielimu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mchungaji Emmanuel Mboje wakiwa ukumbini wakati wa kongamano hilo
Mwalimu wa Injili/Mwinjilisti Happiness
Mwaja Kihama ambaye ni mlezi wa wanafunzi walioandaa kongamano hilo
akizungumza ukumbini jinsi alivyopata maono na kuamua kuhamasisha
wanafunzi wa vyuo mkoani Shinyanga kupitia kwa wakuu wa wakuu wa vyuo
kuungana ili kufanikisha kongamano hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza kwa makini mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama
Mwalimu wa Injili/Mwinjilisti Happiness
Mwaja Kihama alisema lengo la kongamano hilo ni kutengeneza umoja wa
wanavyuo mkoani Shinyanga,kuomba kwa ajili ya elimu mkoani humo na
kuwaombea wanafunzi wote mkoani Shinyanga
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa somo kuhusu “Funguo za Kiagano za Kupata Majibu ya Maombi yetu”
Wanafunzi wa vyuo wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akiendelea kutoa somo ambapo aliwataka wanafunzi kumtegemea mungu
ili kufanikiwa katika masomo na maisha yao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro aliwapongeza wanafunzi hao kuungana pamoja kuuombea mkoa wa
Shinyanga kwani yatasababisha wawe na hofu ya mungu ili kusaidia
kupunguza vitendo vya uovu katika jamii
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwasisitiza wanafunzi hao kujitahidi kusoma na kuachana na tamaa zisizofaa
Mchungaji Goodluck Mosha akiomba ukumbini wakati wa kongamano maalum la maombi kwa wanafunzi wa vyuo mkoani Shinyanga
Wanakwaya ya Haleluya kuu ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga wakicheza ukumbini
Uimbaji unaendelea
Wanachuo wakiimba na kucheza
Vijana wakicheza
Kijana Gabriel akiimba
Vijana wakimwimbia bwana
Uimbaji unaendelea
Wanavyuo wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Wanachuo wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Wanachuo wakiimba ukumbini
Vijana wa TYCS wakiimba ukumbini
Washiriki wa kongamano hilo wakicheza ukumbini
Kongamano linaendelea
Tunafuatilia kinachoendelea
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama
akiongoza maombi kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu kwani hali ya
kitaaluma ipo chini ukilinganisha na mikoa mingine
Wanafunzi wakiwa wamenyoosha mikono wakati wa maombi
Washiriki wa kongamano wakiwa wamenyoosha mikono
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama
akiomba wakati wa kongamano hilo la maombi maalum kwa wanafunzi wa vyuo
vya mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akiwa katika maombi
Maombi yanaendelea
Wanafunzi wakiwa katika maombi
Maombi yanaendelea
Maombi yanaendelea
Maombi yakiwa yamekolea kuombea mkoa wa Shinyanga
Watumishi wa mungu wakiwa katika maombi
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiendelea kuomba
Maombi yanaendelea
Maombi yakiendelea
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama
akiombea wanafunzi wa vyuo na wanafunzi wa shule za sekondari
waliohudhuria kongamano hilo
Maombi yanaendelea
Wanachuo wakiendelea kumsifu bwana Yesu kwa nyimbo
Kulia ni mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya Kongamano hilo Jepherson Jackson akizungumza wakati wa
kufunga kongamano hilo ambapo aliwashukuru watu wote waliofanikisha
kongamano hilo na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana na mlezi wao
Happiness Mwaja Kihama ili kuandaa kongamano jingine
Mchungaji Emmanuel Mboje akizungumza
wakati wa kufunga kongamano hilo ambapo aliwataka wanafunzi hao
kupendana na kuhakikisha wanakwenda kusali na kumuomba mungu
Picha ya pamoja mgeni rasmi na kamati iliyofanikisha kongamano hilo
Kamati iliyofanikisha kongamano hilo
ikiongozwa na mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama ambaye pia ni
mkurugenzi wa EasyFlex Production wakiwa katika picha ya pamoja baada
kumalizika kwa kongamano hilo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment