Ijumaa
Februari 10,2017 kumefanyika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi
wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu Kwa Watoa Msaada wa Kisheria
katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga.
Kikao hicho kilichoandaliwa na
shirika lisilo la kiserikali la Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESH)
linalohusika na utoaji wa msaada wa kisheria kimefanyika katika ukumbi
wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hicho
mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga alipongeza jitihada zinazofanywa
nan a PACESH katika kupinga ukatili wa kijinsia na kusisitiza kuwa
serikali inatambua uwepo wao na itaendelea kuwaunga mkono katika vita
dhidi ya ukatili wa kijinsia.
“Kazi yenu ni
nzuri,kinachotakiwa sasa ni kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wananchi
ili wajue haki zao ili wanapopata matatizo wajue nini cha
kufanya”,alieleza Matiro.
Aidha alisema elimu kuhusu haki
za wananchi pia inatakiwa kutolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa
kwani kama viongozi watakuwa na uelewa wa kutosha itasaidia kumaliza
tatizo la ukatili wa kijinsia.
“Bado watoto wanabakwa,wanapewa
ujauzito,wanawake wanapigwa,wananyimwa haki zao,ili tuweze kumaliza
tatizo la ukatili wa kijinsia ni lazima wadau wote waungane,bila
ushirikiano hatuwezi kumaliza tatizo hili”,aliongeza Matiro.
Kikao hicho mbali na kujadili
masuala mbalimbali yanahusiana na ukatili wa kijinsia pia jumla ya
kompyuta mpakato (laptop) sita zimekabidhiwa kwa wasaidizi wa kisheria
katika vituo vya usaidizi wa kisheria mkoani Shinyanga.
Kompyuta hizo zimetolewa na
shirika mama la Usaidizi wa Kisheria la Legal Service Facility (LSF) la
lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam.
Akizungumzia kuhusu kompyuta
hizo,Meneja Miradi wa shirika la PACESH John Shija alisema zimelenga
kusaidia katika shughuli za kiutendaji katika vituo vya usaidizi wa
kisheria.
Tazama picha 20 za matukio wakati wa kikao hicho..Picha zote na Kadama Malunde -Malunde1 blog
Mgeni rasmi katika kikao cha
Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu
Kwa Watoa Msaada wa Kisheria katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu
mkoani Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa kupinga
ukatili wa kijinsia wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo aliwataka
wananchi kuwa wanajitokeza kutoa ushahidi katika kesi kutokana na kuwepo
taarifa kuwa kesi nyingi zimekuwa zikishindwa kuendelea kutokana na
ushahidi kukosekana.
Mkurugenzi wa shirika la PACESH
Perpetua Magoke akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alisema
shirika lake limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga
dhidi ya ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa shirika la PACESH
Perpetua Magoke alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kutokuwa waoga
kuwafichua watu wanaofanya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani
kukaa kimya kunasababisha vitendo vya kikatili kuendelea kujitokeza
katika jamii
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika
la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akizungumza katika kikao hicho ambapo
alisema ni wakati mzuri sasa wananchi wakabadilika na kutoa taarifa
kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika familia zao na jamii
kwa ujumla
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akisisitiza jambo ukumbini
Meneja Miradi shirika la PACESH
John Shija akielezea kuhusu mradi wa Kuimarisha Uendelevu wa wasaidizi
wa kisheria katika wilaya za mkoa wa Shinyanga
Meneja Miradi shirika la PACESH
John Shija akiendelea kuelezea kuhusu mradi wa Kuimarisha Uendelevu wa
wasaidizi wa kisheria katika wilaya za mkoa wa Shinyanga
Meneja Miradi shirika la PACESH
John Shija alisema miongoni mwa malengo ya mradi huo ni kuongeza
upatikanaji wa huduma bora ya msaada wa kisheria katika jamii mpaka
kufikia mwaka 2021
Malale Johola kutoka Dawati la
jinsia wilaya ya Shinyanga akielezea namna dawati hilo
linavyoshughulikia kesi mbalimbali zinazohusu ukatili wa kijinsia dhidi
ya watoto na wanawake
Malale Johola kutoka Dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga akiendelea kutoa taarifa
Mwenyekiti wa dawati la jinsia
na watoto wilaya ya Kishapu Rose Mbwambo akitoa taarifa kuhusu masuala
ya ukatili wa kijinsia ambapo alisema kesi nyingi zimekuwa zikifutwa
kutokana na kukosekana kwa ushahidi hali inayosababisha vitendo vya
ukatili viendelee kujitokeza katika jamii
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini
kutoka PACESH Pendo Mgeta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema
bado jamii haijawa na uelewa kuhusu haki zao huku akiitaka jamii kuacha
uoga kuwafichua wahusika wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na
watoto
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka PACESH Pendo Mgeta
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro(kulia) akimkabidhi Kompyuta mpakato bwana Buyamba
Ngogeja kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria katika kituo cha usaidizi wa
kisheria wilaya ya Kishapu.Laptop hizo zimetolewa na shirika mama la
Usaidizi wa Kisheria la Legal Service Facility (LSF) la lenye makao
makuu yake jijini Dar es salaam.
Wasaidizi wa kisheria katika
kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya ya Shinyanga wakipokea
laptop.Aliyevaa suti kushoto ni bwana Deogratius Kashindye akishikana
mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda
Bi Sophia Malimo kutoka Manispaa ya Shinyanga akipokea laptop kwa ajili ya kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya hiyo
Bi Sophia Malimo kutoka Manispaa ya Shinyanga akishikana mkono na meneja miradi kutoka PACESH John Shija wakati akipokea laptop
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment