Wednesday, February 1, 2017

FEMINA HIP YAWAJENGEA VIJANA NCHINI UWEZO WA UONGOZI NA KUJIAMINI.


imagesNa: Frank Shija – MAELEZO
FEMINA Hip yatoa tuzo tano za mwaka kwa Klabu za Fema ambazo zimefanya vizuri katika Nyanja mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang wakati wa Kongamano la mwaka la Vijana leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa tuzo hizo zinatolewa ili kutia chachu kwa vijana kuongeza bidi katika kutatua changamoto zao kwa kujiamnini huku wakiwa na ujuzi mwepesi utakaowaomgezea umakini katika shughuli zao.

“Tmezigawa tuzo hizi katika makundi makuu matano ambayo ni Mtandao Bora wa Klabu ya Fema ambayo imekwenda kwa Mwanza Federation Fema Clubs, Mshindi wa Pili wa Mtandao Bora wa Klabu za Fema iliyochukuliwa na Dodoma Students and Teachers”.Alisema Fuhlesang.
Tuzo zingine kuwa ni Mhamasishaji Bora wa Mtandao wa Klabu za Fema wa mwaka iliyokwenda kwa Mwalimu Christopher Mavunde, Mhamasishaji Bora wa Klabu za Fema wa mwaka iliyochukuliwa na Mwalimu Bryson Paul kutoka Ngweli FEMA Klabu – Shule ya Sekondari Ngweli wilayani Sengerema pamoja na Klabu bora ya FEMA kwa mwaka ambayo ni Kisihigh Fema Club kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri mkoani Arusha.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi huyo amesema kuwa FEMINA Hip imekuwa ikiendesha program za kuwakutanisha vijana ili kuwajengea uwezo katika Nyanja za mabalimabali ikiwemo uongozi kwa manufaa ya sasa na baadae.
Ujuzi ambapo vijana wamekuwa wakipatiwa kutoka kwa wataalamu wa Shirika hilo ni pamoja na mawasiliano,mabadiliko ya mitazamo,elimu juu ya afya ya uzazi, malezi na makuzi pamoja na stadi za maisha.
Kwa upande wake mshindi wa tuzo  Mhamasishaji Bora wa Klabu za Fema wa mwaka 2017 Mwalimu Bryson Paul amesema kuwa Klabu za FEMA zimekuwa msingi imara wa kuwajengea uwezo wa kujitambua vijana wengi nchini hivyo ni vyema watanzania wakatambua umuhimu wa vijana wao kushiriki katika vikundi hivyo ambavyo vimekuwa na lengo la kuwajengea uwezo kwa kuwapa elimu na ujuzi mbalimbali ikiwemo stadi za maisha.
Aliongeza kuwa binafsi amefarijika kwa kuibuka kuwa mshindi katika kipengele hicho na kusisitiza kuwa siri pekee ni nidhamu na moyo wa kujifunza Zaidi kwa kushirikiana na wenzako.
FEMINA Hip imewakutanisha vijana walikatika Klabu za FEMA kutoka pande zote za nchi katika Kongamono lililofanyika katika hoteli ya Belinda Jijini Dar es Salaam, ambalo pamoja na utoaji wa tuzo pia vijana walipata fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu elimu na masuala mtambuka kwa vijana.

No comments :

Post a Comment