Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi (anayeangalia kamera) akimpatia Nya Mathias shilingi
34,500 kama malipo ya kuchimba bwawa kwa siku 15 ambapo kila siku
anapaswa kulipwa shilingi 2,300. Fedha hizo zimetolewa na TASAF 111 kwa
ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia miradi ya jamii iliyoibuliwa na
walengwa wa TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi akiangalia bwawa linaloendelea kuchimbwa na kaya maskini
za kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba kupitia TASAF 111. Mkuu huyo wa
mkoa ameagiza halmashauri zote zisaidie kutoa fedha ili ujenzi wa
mabwawa yaliyoibuliwa na kaya masikini yaweze kukamilika kwa muda mfupi.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge
wilaya ya Iramba Mkoani Singida Stephano Mkiya akizungumza muda mfupi
kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini
amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kuanzisha ufugaji wa mbuzi na
pia anamudu kuwasomesha watoto wake.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge
wilaya ya Iramba Mkoani Singida Elizabeth Mkumbo akizungumza muda mfupi
kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya
maskini, Elizabeth amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kujenga nyumba
bora ya mabati na kwa sasa ana uhakika wa chakula tofauti na kipindi
hajaunganishwa na mpango wa TASAF.
Mratibu wa TASAF Mkoani Singida
Patrick G. Kasango akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la uhaulishaji
wa fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini 146 katika kijiji cha
Kikonge wilaya ya Iramba mkoani hapa. Kwa mujibu wa Kasango hadi sasa
kaya 39,102 maskini Mkoa wa Singida zimenufaika kwa kupatiwa zaidi ya
shilingi bilioni 20.3.
…………………………………………………………………………..
Na Gasper Andrew- Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi ameagiza maafisa mifugo kata kusimamia kwa karibu miradi
ya ufugaji kuku na mbuzi inayotekelezwa na kaya maskini zilizopo kwenye
mpango wa TASAF 111.
Amesema kuku au mbuzi katika
miradi hiyo wakifa kwa kukosa huduma kutoka kwa maafisa mifugo,maafisa
hao watalazimika kufidia kuku au mbuzi hao watakaokufa.
Akilijengea nguvu agizo lake hilo
Dkt. Nchimbi alitoa kutoka mfukoni kwake shilingi 150,000 taslimu na
kumpatia afisa mifugo kata ya Kikonge Wilayani Iramba kwa ajili ya
kuikarabati pikipiki yake iweze kumrahihishia kufika kwenye miradi ya
kaya maskini.
Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo
juzi muda mfupi baada ya kumaliza kukagua bwawa la kijiji cha Kikonge
wilaya ya Iramba linalojengwa kwa nguvu za kaya maskini.
Amesema serikali pamoja na wadau wanaotoa fedha kwa kaya maskini,ili ,ziweze kujikwamua kutoka lindi la umaskini.
“Njia mojawapo ya kuzisaidia kaya
hizi maskini kuboresha vipato vyao,ni hii ya miradi midogo midogo ya
ufugaji kuku,mbuzi na mifugo meinge.Ninyi maafisa mifugo ambao mpo
karibu na kaya hizi,zisimamieni kikamilifu,msisubiri mfuatwa,ninyi ndio
muifuate miradi huko iliko”,alisisitiza.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa,
amewataka watendaji hao wahakikishe wana simamia watoto wa kaya maskini
wana hudhuria shuleni bila kukosa.
“Serikali inaamini hawa watoto
wa kaya maskini ambao TASAF inagharamia masomo yao, ndiyo watakao kuja
kuwa mtaji kwa kaya maskini kujikomboa kiuchumi. Kwa hiyo upo umuhimu
mkubwa wa kusimamimiwa na kuhimizwa kusoma kwa bidii”,alifafanua.
Mkuu huyo wa mkoa, pia amewataka
walimu watambue kwamba wana fundisha watoto ambao wengine wakiwa ni wa
kaya maskini,.Kwa hali hiyo, mchango wao unatakiwa katika kuwa jengea
misingi itakayo weza kusaidia kuzikomboa kiuchumi kaya zao.
Awali mratibu TASAF mkoa wa
Singida, Patrick Kasango, alisema mpango wa kunusuru kaya maskini
(PSSN) unatekelezwa na TASAF 111, katika wilaya zote sita za mkoa huu.
Alisema mpango huo ulianza na kaya 39,426, lakini kutokana na sabaubu mbalimbali hadi sasa zimebaki kaya lengwa 39,102.
“kaya hizi maskini zimewezeshwa
kupata mahita ya msingi ikiwemo chakula hasa wakati wa njaa, mahudhurio
shuleni yameboresha kwa wanafunzi na kuboresha afya za watoto wadogo
wanaodhuziria kliniki.Kwa kifupi,hadi januari mwaka huu, zaidi ya
shilingi 20.3 bilioni, zimehawilishwa kwa kaya masikini mkoani
kwetu”,alisema Kasango.
Wakati huo huo Mmoja wa
wanaufaikaji wa mpango huo wa TASAF 111,Elizabeth Mkumbo,amesema
amefanikiwa kujenga nyumba bora,kuwa na akiba na kuanzisha ufugaji wa
kuku kupitia fedha za mradi wa TASAF 111.
No comments :
Post a Comment