Diwani
wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) akishirikiana na Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala,Msongela Palela na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Edward
Mpogolo (kulia) wakifanya usafi katika maeneo ya buguruni kwa malapa
kutimiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa
wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela akizungumza na wananchi wa eneo la
Buguruni kwa Malapa na Darajani kuhusu kufanya usafi katika maeneo
yanayowazunguka ili kujikinga na kujiepusha na magonjwa ya milipuko kama
Kipindupindu baada ya kufanya
usafi kutekeleza agizo la Rais Dk.John
Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es
Salaam juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) na
Katibu tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo.
(PICHA NA ELISA SHUNDA)
………………………………………………………………
NA EMERISIANA ATHANAS
DIWANI
wa Kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Adam Fugame
ameagiza viongozi wa kata akiwemo Ofisa Afya, kuwakamata na kuwachukulia
hatua watu wasiofanya usafi au kuchangia kwaajili yakuzolewa uchafu.
Akizungumza
jijini hapa jana, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ulioshirikisha
viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilala akiwemo Mkurugenzi Msongela
Palela, alisema ni vema viongozi wakafanya kazi kwa mujibu wa sheria ili
kuwashughulikia watu hao.
“Suala
hili sio rai bali tufanye kama sheria ili kufanikisha zoezi la
kuimarisha usafi katika maeneo yetu, kwani tusipofanya hivi hakuna
litakalotekelezwa, watu hawafanyi usafi,” alisema.
Kutokana
na umuhimu wa kufanya usafi alisema ni vema watakaokutwa hawachangii
wala kujishughulisha na kufanya usafi wakachukuliwa hatua na kutozwa
fedha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Palale alisema kuwa katika
kata tisa zilizoko katika manispaa hiyo kata ya Buguruni ndiyo imekuwa
na ugonjwa wa kipindu pindu ambacho husababishwa na hali ya uchafu.
Alitumia
nafasi hiyo kuwataka wakazi wa kata ya Buguruni kuhakikisha wanafanya
usafi na kuwa walinzi katika kuhakikisha wanalinda mazingira na
kuimarisha usafi kwenye maeneo yao
No comments :
Post a Comment