Tuesday, February 28, 2017

COLLINS SALIBOKO APANIA KUSHINDA MEDALI KWENYE MASHINDANO YA VIJANA YA JUMUIYA YA MADOLA


01
Collins Saliboko akijaindaa ‘ku-dive’ au kuchupa katika bwawa la Chuo cha St Felix, Uingereza)
02
Muogeleaji wa Tanzania, Celina Itatiro akichupa kwenye mashindano ya Afrika Kusini
03
Collins Saliboko akichapa maji St Felix College, Uingereza.
04
Celina Itatiro (Mwenye kofia ya orange) akiogelea huku akiwa na glasi ya maji kwenye paji la uso.
05
Collins Saliboko (wa kwanza kulia) akiwa na waogeleaji wa Tanzania wanao soma St Felix College; Aliasgar Karimjee na Sonia Tumiotto mara baada ya kutwa medali katika mashindano ya chuo.
Na Mwandishi wetu
Muogeleaji chipukizi wa Tanzania, Collins Saliboko ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ya Vijana  ameahidi kuipeperusha vyema na kuiweka histori katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Mbali ya Collins ambaye anashindana kwa upande wa wanaume, msichana, Celina Itatiro ataiwakilisha nchi kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika nchini Bahamas kuanzia Julai 18 mpaka 23 kenye mji wa Nassau.
Collins ambaye kwa sasa anasoma Chuo cha St Felix, Uingereza, amesema kuwa ameanza mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo chini ya kocha wake, Sue Purchase amesema kuwa amepania kufanya kile ambacho watanzania wengi hawatakitarajia kupitia mchezo wa kuogelea ambao kwa sasa unakuja juu kwa kasi.
Alisema kuwa atatumia pia mazoezi ya timu ya kuogelea ya chuo chao kama sehemu ya maandalizi, kabla ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ambayo itatangazwa hapo baadaye.
“Naahidi kuitendea haki nafasi hii, hii inatokana na juhudi zangu katika mchezo wa kuogelea, matokeo yangu bora ndiyo yamenipa nafasi hii, naona mwanga katika mchezo wa kuogelea na ninaahidi kufanya vyema,”
“Mazoezi ya hapa St Felix ni mazuri sana, hii inatokana na vifaa bora na walimu wazuri, hapa ia kuna ushindani mkubwa na hivi juzi  juzi tu nilishinda nafasi ya pili kwenye mashindano ya huku Uingereza, ni matokeo mazuri na ninaahdi kufanya vyema zaidi,” alisema Collins kwa njia ya simu.
Alisema kuwa mpaka sasa ameshiriki katika mashindano mengi ya ngazi ya chuo na kupata matokeo mazuri. “Mashidano haya ya Chuo ni sehemu ya maandalizi yangu, naishi hapa chuoni, kila Napata muda mwingi wa kujifunza, Mwalimu wangu, Sue ni mkali na kwa sasa anajua jukumu langu la kitaifa, ameongeza ‘dozi’ ya mazoezi,” alisema.
Katibu Mku wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alisema kuwa kazi iliyopo sasa ni kwa makocha kuwaandaa wachezaji katika matukio watakaoshiriki ili kuweza kufanya vizuri.
Namkoveka alisema kuwa mbali ya kusaka medali, lengo kuu la chama kwa wachezaji hao ni kupunguza muda wao ili baadae waweze kufikia muda unaotakiwa na  Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani, (FINA) kiwango cha muda B au A.
 Mashindano ya jumuiya ya madola haya yatakuwa ya sita baada ya kuanzishwa kwake mwaka 2000 na wakitegemewa vijana 1000 wenye  umri wa miaka kuazia maika 14 hadi 18  kushindana katika michezo mbalimbali.

No comments :

Post a Comment