Habari tulizozipata hivi punde
kutoka mkoani Kilimanjaro zinasema kuwa watu zaidi ya watatu wamefariki
dunia akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo Anord Swai na
mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai katika ajali ya
gari dogo.
Inaelezwa kuwa ndani ya gari walikuwemo watu sita wakiwemo
viongozi wa CCM wakitoka kushiriki sherehe za miaka 40 ya CCM kimkoa
yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Shauri Tanga wilayani
Rombo.
Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa ni fuso kufeli breki na kuligonga gari dogo.
“Waliofariki ni mwenyekiti wa Uvccm wilayani hai na mwandishi wa habari Leo Arnold Swai, mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT mkoa wa Kilimanjaro ally Mmbaga na wanafunzi makada wa CCM kutoka vyuo vikuu vya ushirika na KCM. Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo amekimbizwa Hospitali na wote walikuwa wakitoka kwenye maadhimisho ya kilele cha miaka 40 ya kuzaliwa CCM wilayani Rombo” -Ujumbe wa mwandishi wa habari Lucy Ulomi ambaye sasa yupo hospitali ya KCMC akifuatilia habari hiyo.

CHANZO MALUNDE1BLOG
No comments :
Post a Comment