Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula baada ya
kuwasili kwenye jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kufungua
jengo hilo Januri 21, 2017. Mangula ni mkazi wa eneo hilo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa Kiwanda cha Chai cha Kibena
wilayani Njombe baada ya kukitembelea Januari 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifungua jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika
eneo la Igwachanya Januari 17, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa
wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe baada ya
kuweka jiwe la msingi la jengo hilo katika eneo la Igwachanya , Januari
17, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Kibena wilayani Njombe Januari 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kasisim Majaliwa
akiwasalimia wananchi wa eneo la Igwachanya wilayani Wanging’ombe baada
ya kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Januari 21,
2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ilembula wilayani Wanging’ombe Januari 21, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama ngoma ya wasanii wa eneo la Wikichi wilayani Njombe wakati
alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Rufaa ya
Mkoa huo, Januari 21, 2017.Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Christopher `Ole Sendeka.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema jumla ya vijiji 53 vya mkoa wa Njombe vitapatiwa huduma ya maji
safi na salama katika mwaka huu wa fedha.
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi,
Januari 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya
Wanging’ombe katika mkutano wa hadhara katika kata ya Ilembula.
Waziri Mkuu alisema zaidi ya sh.
bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia mradi huo wa maji katika
miji ya Makambako, Njombe na wilaya ya Wanging’ombe.
Alisema kati ya vijiji hivyo
vitakavyopatiwa maji, vijiji 22 ni vya wilaya ya Wanging’ombe, hivyo
aliwaomba wananchi hao kuwa na subira.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu tayari
zabuni ya mradi huo imeshatangazwa, hivyo amewaagiza viongozi wa Wizara
ya Maji na Umwagiliaji watafute mkandarasi mzuri.
Alisema lengo la Serikali ya Awamu
ya Tano ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji katika
umbali usiozidi mita 400 kutoka mahali anapoishi.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo
baada ya Mbunge wa Wanging’ombe, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Lwenge
kumuomba awasaidie katika kutatua kero ya maji.
Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri
wa Maji na Umwagiliaji alisema “Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi tunakabiliwa
na changamoto ya maji, leo tunaomba ututatulie kero hii”.
Changamoto nyingine aliyoitaja
Mheshimiwa Lwenge ni pamoja na ukosefu wa hospitali ya wilaya, ambapo
Waziri Mkuu aliigiza halmashauri hiyo kuanza ujenzi.
Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2015/2020 inaelekeza kuwa na hospitali katika kila wilaya,
kituo cha afya kwa kila kata na zahanati kwa kila kijiji.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Ally Kasinge kukutana na viongozi wa
kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Mapanga Kipengele ili kutatua
kero ya mpaka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.
No comments :
Post a Comment