Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye mara baada ya
kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja kwa ajili ya kufungua sherehe za
maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China leo jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mamia ya wakazi
wa Jiji la Dar es Salaam leo wakati hafla ya kufungua sherehe za
maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China.China
inasherehekea Mwaka Mpya ambapo mwaka huu umepewa jina la Jogoo
(Rooster).
Balozi wa China nchini Tanzania
Balozi Dkt. Lu Youqing akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (wapili kutoka kulia)
akiwaongoza viongozi na wananchi kuimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla
ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho yam waka mpya wa China leo jijini
Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Nape Moses Nnauye, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.
Augustine Mahiga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini
Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa
sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vikundi mbalimbali vya
burudani kupitia Sanaa wakionyesha umahiri wao wakati wa hafla ya
uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar
es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya
shilingi milioni 70 na laki nne kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi
Chato kutoka kwa Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla
ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa
maadhimisho hayo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea
katika hafla ya kuadhimisha mwaka mpya wa China leo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya washiriki wa
maadhimisho hayo wakitembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika viwanja
vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yam waka mpya wa China
leo jijini Dar es Salaam. China wanasherehekea mwaka mpya leo na kesho
katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 11
jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa China
hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa
sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es
Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja
kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na yanatarajiwa kumalizika
kesho tarehe 22 Januari 2017.
Picha zote na: Frank shija & Shamimu Nyaki
No comments :
Post a Comment