Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni wake
ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF,
Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo
Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara
hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya
Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia)
akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa
mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini
Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia vizuri ukuaji
wake wa uchumi.
Ujumbe wa Tanzania na Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani-IMF wakiwa katika mazungumzo Makao Makuu ya
Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ambapo Shirika hilo
limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kufikia maendeleo
inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake kiuchumi na
kijamii.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia)
akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo
Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia
kikamilifu ukuaji wake wa uchumi.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ollal, akisisitiza jambo wakati wa
mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw.
Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni wake ambaye ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw.
Bhaswar Mukhopadhway, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao
yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, ambapo
IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, katika kusimamia na
kukuza uchumi wa Taifa.
……………..
Benny Mwaipaja,WFM-Dar es salaam
SERIKALI imesema kuwa
inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi
na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili
kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.
Hayo yamesema na Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw.
Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa uchumi wa nchi
unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo
itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na
ulipaji kodi.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway,
amesema kuwa Shirika lake limeridhika na kiwango kikubwa cha ukuaji wa
uchumi wa Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia
kuona uchumi huo ukiendelea kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta
binafsi.
Ametaja sifa za ukuaji huo kuwa ni
pamoja na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi, udhibiti wa mfumuko wa
bei na thamani ya shilingi, uwajibikaji na pamambano dhidi ya rushwa,
ufisadi, na utekelezaji mzuri wa Bajeti ya serikali.
Hivi karibuni Bodi ya Wakurugenzi
ya IMF ilitoa taarifa yake ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania
na kueleza kuridhika kwake na uimara wa uchumi huo baada ya kutoyumba
katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na kueleza kuwa utaendelea kukua kwa
wastani wa asilimia 7 kama ilivyopangwa.
Shirika la Kimataifa la Fedha
Duniani ni chombo cha kimataifa kinachosaidia ukuaji wa uchumi wa nchi
wanachama wake kwa kuweka mikakati na kuzikopesha fedha kwaajili ya
shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchmi na kijamii ikiwemo, elimu,
afya, miundombinu, nishati na miradi mingine kadha wa kadha
No comments :
Post a Comment