Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi
la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara
ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi
hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari
lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu kutoka kwa Mrakibu
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha
mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza
maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini
Kaizaga, juu ya gari lililokamatwa likisafirisha madawa ya
kulevya.Wengine mstari wa mbele ni Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya
Emmanuel Lukula(wapili kulia) na Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio
Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo
wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi
katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya
mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la
Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments :
Post a Comment