MTOTO ADAIWA KUMUUWA BABA YAKE MZAZI KISHA KUCHIMBA SHIMO LA KUTAKA KUMZIKIA
Mwenye tishert ya damu ya mzee ni Pius Malindisa ambaye ni mdogo wake marehemu.
Nyumbani kwa kwa marehemu ATANAS PATRICK watu wakiwa wamejitokeza kwa ajili ya kwenda kumstili.
Na Amon Mtega
JESHI la polisi mkoani Ruvuma
linamshikilia Patrick Malindisa [29 makazi wa mtaa wa Namanyigu kata ya
Mshangano Manispaa ya Songea mkoani humo kwa tuhuma za kumuua baba yake
mzazi Atanasi Malindisa [70] kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu
kichwani na kidevuni upande wa kushoto kisha kufanya jaribio la kuchimba
shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya kumzikia baba huyo.
Akizungumza na Ruvuma TV
katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu
Piusi Malindisa alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao
Januari Mosi mwaka huu majira ya 1.30 kutoka kwa mtoto wa marehemu
Patrck Malindisa .
Piusi alisema kuwa mtoto huyo ambaye
alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na marehemu huyo alitoa taarifa kwa
wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo na ndugu walipofika
kabla ya kuingia chumbani alikokuwa akilala marehemu waliamua kuuita
uongozi wa mtaa ambao uliingia na kubaini kuwa Atanasi Malindisa
ameuwawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni.
Alisema kuwa baada ya kubaini hilo
walitoa taarifa polisi kisha mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuuhifadhi
Hospital ya mkoa Ruvuma [HOMSO] kwa uchunguzi huku jeshi la polisi
likimshikilia mtoto wa marehemu kwa mahojiano zaidi.
Alifafanu kuwa polisi wakiwa bado kwenye
nyumba hiyo walibaini kuwa kwenye moja ya chumba ambacho hakijaezekwa
kulichimbwa shimo linaloendana na vipimo vya marehemu ambalo lilihisiwa
kuwa alitaka amfukie humo ili watu wasijue kwa kuwa kwenye nyumba hiyo
walikuwa wakiishi wawili.
“Uchimbaji wa shimo hilo lenye mithiri ya
kaburi lilimshinda kisha akamua kulifukia na kuchukua hatua ya kuja
kutoa taarifa kwetu wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo
ambayo inadaiwa alikuwa akilia nalo kumbe sivyo bali kapigwa na kitu
kichwani”alisema Ndugu wa marehemu.
Kwa upande wake jirani wa nyumba hiyo
ambaye hakutaka kulitaja jina lake alisema kuwa maisha ya marehemu na
mtoto wake walikuwa wakipigana mara kwa mara hasa kwa kutumia silaha na
majirani walikuwa hawapo karibu nao kutokana na tabia hizo.
Vituko vya tawala kwenye makaburi ya
Namanyigu wakati wa uchimbaji wa kaburi la kumzikia marehemu Atanasi
Malindisa ambako mtandao huu umeshuhudiwa vijana walitaka kugomea
kuchimba kaburi hilo kwa madai kuwa familia hiyo ilikuwa haijihusishi
kwenye matatizo ya majirani.
Baadhi ya wazee waliwasii vijana hao kwa
kuwaomba wasilipe ubaya kwa ubaya cha msingi wafanikishe kumuhifadhi
marehemu kwa kuwa marehemu hayupo duniani hivyo ni vema wakasamehe na
kumuachia Mungu.
Katika usafirisaji wa mwili huo kutoka
katika Hospital ulikohifadhiwa baada ya magari ya maeneo hayo
kutokuonyesha nia ya kutoa msaada gari la Mbunge wa jimbo la Songea
mjini Leonidas Gama ambalo alilitoa kwa wananchi kwaajili ya matatizo
mbalimbali la okoa jahazi kwa kuubeba mwili wa marehemu huyo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma
Zuberi Mwombeji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na
kumshikilia mtuhumiwa Patrick Malindisa mtoto wa marehemu na kuwa jeshi
hilo linaendelea na upelelezi likiwemo shimo lililokutwa.
No comments :
Post a Comment