Monday, January 2, 2017

KAYA MASKINI 704 ZAONDOLEWA KWENYE MPANGO WA TASAF KUNUSURU KAYA MASKINI


tasa
 Na Mahmoud Ahmad Arusha
JUMLA ya kaya 704 mkoani Arusha ambazo hazina sifa zimeondolewa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini  unaotekelezwa kupitia TASAf ,a kuagiza uhakiki zaidi ufanywe ili kubaini kaya zilizoingizwa kwenye mpango huo zikiwa hazina sifa ziondolewe mara moja.
 
, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ,Richard Kwitega,ameyasema hayo Desemba 27 mjini Loliondo, wilayani Ngorongoro, kwenye kikao cha kutathimini utekelezaji wa TASAF awamu ya tatu pamoja na Programu ya OPEC awamu ya tatu ambapo mipango yote hiyo inalenga kuzisaidia kaya masikini kujikwamua kiuchumi.
 
Akizungumza kwenye kikao hicho cha kazi chawatendaji wote wa TASAF mkoani Arusha, Katibu tawala huyo ameagiza watendaji wote waliohusikakuingiza kaya  zisizo na sifa kwenye mpango huo wachukuliwe hatua za kinidhamu ikiwemo kurejesha fedha hizo ili zitumike kusaidia sehumu nyingine
 
 
Amesema jumla ya kaya 44643 ziliandikishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015  na zilistahili kupata Malipo ya kwanza mwezi Julai na Augosti mwaka 2015  ambapo zilipokelewa jumla ya shilingi 1,854, 369,500 .
 
Amesema mpaka sasa mkoa umepokea  awamu tisa za malipo ya ruzuku kwa kaya masikini ambapo shilingi 17,159,438,634 zimeshapokelewa na kati ya hizo  shilingi 15328653294 zimehaulishwa kama ruzuku kwa walengwa huku shilingi 1,830, 785 339 zimetumika  kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji  wa shughuli za mpango  huo.
 
Kwitega, amesema  mwezi Mei mwaka 2016 serikali ilipokea  ujumbe wa benki ya dunia  na kufanya nao mazungumzo juu ya makundi  yanayoishi kwenye mazingira  magumu  ikiwa ni kuangalia utekelezaji wa mpango wa kunusuru makundi maalumu.
 
Ameongeza kuwa ujumbe huo umetembelera wilaya ya Karatu,mkoani Arusha ili kuona,kuzungumza na walengwa  ili kuonas makabila yanayoishi kwenye mazingira magumu wilayani humo yanaandikishwa kwenye mpango huo wa kunusuru kaya masikini.
Tayari kaya 2080 zimeandikishwa  wilayani Karatu katika tarafa ya Eyasi kuanzia Augosti 2016
 
Kwitega, amesema pamoja na mafanikio ya TASAF awamu ya tatu bado yapo maeneo ambayo wananchi wanahitaji kusaidiwa katika kujikwamua na umaskini uliokisiri.
 
 
Kwa upande Kaimu Mkurugenzi wa TASAF Omari  Malilo,  amezitaka halmashauri za wilaya kukamilisha  miradi hiyo kabla ya mwezi Februari, 2017.
 
Programu hiyo inaendeshwa  ndani mpango wa kunusuru kaya makini (TASAF,111ambayo vijiji na mitaa  iliyopo kwenye mpango huo  ilizinduliwa rasmi kitaifa mkoani Arusha, mei 3 mwaka 2015  ambapo nchini program hiyo inatekelezwa  kwenye mikoa miwili ya Arusha na Njombe kwa ufadhili wan chi  zinazozalisha na kuuza mafute Ulimwenguni OPEC,
 
Ambapo wananchi wamekuwa wakiibua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu, Elimu, Afya .
 
 Ambapo mkoa wa Arusha katika kutekeleza mpango ghuo umeibua jumla ya miradi 63 na tayari shilingi 1,556, 709, 896 zimetolewa kupitia TASAF  na miradi 43 ipo katika hatua mbalimbali  za utekelezaji  wake  ambapo jumla ya shilingi 2,748, 468, 978,zimetengwa ili kukamilisha miradi yote 63

No comments :

Post a Comment