Sunday, January 22, 2017

KINANA: CHAGUENI VIONGOZI WATAKAOWASAIDIA SIYO WATAKAOSHUGHULIKA NA SHIDA ZA MATUMBO YAO



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea Udiwani kata ya Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Mwalimu Zakaria Nnko, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mpira vya Shule ya Ngarenanyuki, leo Januari 21, 2017.
Akimnadi Mgombea huyo, Kinana amewataka Watanzania kujenga tabia ya kuchagua  viongozi watakaowasaidia na kuacha kuchagua ambao wakishapata madaraka wanashughulikia shidao za matumbo yao badala ya shida za wananchi waliowachagua.
Alisema, baadhi ya wa wananchi wamekuwa hawatazami sifa na uwezo wa mgombea atakayewatumikia, badala yake kuchagua kwa kukurupuka kuchagua viongozi ambao baadaye hawawasaidii kutatua kero zao, na hivyo kubaki wanalalamikia serikali kuwa haiwahudumii.
Kinana aliwataka wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki kumchagua Mwalimu Nnko, akimwelezea kuwa anamtambua vyema kuwa ni mchapakazi na ni mtu ambaye ameridhika na maisha hivyo anagombea ili kuwasidia wanannchi na siyo kujisaidia yeye kuneemesha tumbo lake.
Uchaguzi mdogo unafanyika katika maeneo mbalimbali nchini, kujaza nafasi zilizobaki wazi kuokana na sababu mbalimbali zilizofanya madiwani na wabunge wlioshinda kutokuwepo. Uchaguzi huo unafanyika chini ya usimamizi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Kijana wa CCM, aliyempa saluti hiyo ya heshima baada ya kumvalisha skafu alipowasili kwenye Viwanja vya Mpira ya Shule ya Msingi Ngarenanyuki, kufunga kampeni hizo leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia ananchi baada ya kumvalisha skafu alipowasili kwenye Viwanja vya Mpira ya Shule ya Msingi Ngarenanyuki, kufunga kampeni hizo leo
Wananchi wakiwa na ujumbe kwnye mabango ambapo alisema wakimchagua mgombea wa CCM, CCM itamsukuma mgombea huyo kuhakikisha wanakopehwa bodaboda
Wananchi wakimshangilia Kinana kwenye mkutano huo
Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria mkutanohuo
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisalimia wananchi kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laizer akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kumnadi Mgombea na kisha kufunga kampeni hizo
Vijana wakiwa kwenye mtiilikufaidi vizuri mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia mkutanohuo
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea Udiwani katika kata ya Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Mwalimu Zakaria Nnko, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, uliofanyika kwenye Viwanja vya  Mpira vya shule ya Ngarenanyuki, leo Januari 21, 2017. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments :

Post a Comment