Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uratibu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi,Jason Kami akiwasilisha mpango wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo. |
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uratibu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi,Jason Kami akiwasilisha mpango wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo. |
Kaimu
Mkurugenzi Wanyamapori nchini,Profesa Alexander Songorwa akizungumza
umuhimu wa uhifadhi na kutenga eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 1,500
kwaajili ya mapito na mazalia ya wanyama.
|
Wadau
kutoka taasisi mbalimbali wakisikiliza kwa makini mawasilisho ya
makundi mbalimbali katika kikao cha kutafuta suluhu ya mgogoro wa Pori
Tengefu la Loliondo.
|
Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakisikiliza kwa makini mawasilisho ya makundi mbalimbali katika kikao cha kutafuta suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo. |
Diwani wa Kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro akiwasilisha maoni ya wenyeji na kuomba serikali iache mpango wake wa kulichukua eneo hilo kwani jamii inalihitaji. |
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ameendelea kuongoza vikao vya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu ambao umechukua muda mrefu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika zaiara yake mwezi desemba mwaka jana alimwagiza Mkuu mkoa kuwakutanisha wadau wote na kupata maoni yao ili kuumaliza kabisa mgogoro huo.
Katika kipindi cha siku saba wajumbe wamekutana na kujadili chanzo na hatua zilizochukuliwa pia wametembelea eneo lilikusudiwa kutengwa kwaajili ya mapito ya wanyama na mazalia ya nyumbu sanjari na kuangalia vyanzo vya maji na miundombinu.
Gambo amesema serikali iko makini kuangalia njia bora za uhifadhi huku wananchi wakiendelea na maisha yao ya ufugaji bila kuathiri sekta ya utalii kwa ujumla huku maslahi ya wawekezaji yakilindwa kwani wana mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya taifa yanayotokana na kodi wanazolipa.
Taasisi mbalimbali zimewakilishwa zikiwemo Tanapa,NCAA,Tawiri,Asasi za kiraia,Jamii ya wananchi wanaoishi Loliondo na serikali ya mkoa na wilaya.
No comments :
Post a Comment