Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao
(kulia), akifungua warsha (mafunzo) ya siku tatu kwa wanatasnia ya
Filamu na Maigizo mkoani Mara, yaliyoanza hii leo katika Ukumbi wa Shule
ya Sekondari Mara iliyopo Musoma Mjini.
Wengine
ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso(katikati)
pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba
(kushoto).
Warsha
hiyo imeandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kupitia Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wanatasnia
ya filamu na maigizo ili kuzalisha kazi zenye ubora (maudhui) na
kuboresha soko la ndani na nje ya nchini, kama kaulimbiu isemavyo,
“Filamu ni Uchumi, Filamu ni Ajira”.
Tayari
warsha ya aina hiyo imefanika mikoa ya Morogoro na Mwanza ambapo pia
itaendelea kufanika katika mikoa mingine nchini ikiwa pia ni utekelezaji
wa kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape
Nnauye, kuhakikisha wizara hiyo inafikisha huduma zake mikoani badala ya
Dar es salaam pekee.
Na BMG
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso (kushoto) akizungumza kwenye warsha hiyo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba akizungumza kwenye
warsha hiyo. Katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini na
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao
Wanatasnia
ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, wakimsikiliza Rais wa Shirikisho la
Filamu nchini, Simon Mwakifwamba wakati akizungumza kwenye warsha ya
mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hao hii leo.
Kaimu
Afisa Utamaduni mkoani Mara, Sheikudadi Saidi, akizungumza kwenye
warsha kwa wanatasnia ya filamu na maigizo mkoani Mara, hii leo.
Mhadhiri
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaa, idara ya Sanaa, Richard Ndunguru,
akitoa semina masuala ya picha nyogevu na uongozaji wa filamu.
Wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaa, idara ya Sanaa, Richard Ndunguru.
Zaidi
ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo
ya filamu na maigizo kutoka Bodi ya Filamu nchini. Pia wawakilishi
kutoka maeneo jirani ikiwemo Simiyu wamehudhuria mafunzo hayo.
Zaidi ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya filamu na maigizo kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akizungumza na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na umuhimu wa mafunzo hayo katika
kuinua tasnia ya filamu na maigizo nchini.
Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara TDFAA, Johnson Ibambai (Dunia), akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa mafunzo hayo.
Msemaji
wa Chama cha Waigizaji wilayani Bunda, Jaqueline Frank (kushoto)
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) na kuipongeza serikali
kupitia Bodi ya Filamu nchini kwa kutoa mafunzo kwa wanatasnia ya filamu
na maigizo ili kuboresha zaidi kazi zao za sanaa.
#BMGHabari
Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini,
imeendelea kuhakikisha inawafikia wanatasinia wa filamu na maigizo
nchini na kuwapatia mafunzo kwa ajili ya kuboresha kazi.
Akifungua
hii leo mafunzo ya siku tatu kwa wanatasinia ya filamu na maigizo
mkoani Mara, Naimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Nuru Milao, amesema hayo
yawe chachu ya uboreshaji wa filamu zinazozalishwa nchini na hivyo
kuingia kwenye soko la ushindani ndani na nje ya nchi.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Jocye Fissoo, amesema Serikali inayo
dhamira ya dhati ya kuhakikisha uchumi wa kati wa viwanda unafikiwa
kupitia filamu ndiyo maana imeamua kutoa mafunzo hayo ambayo yatazalisha
waigizaji, waongozaji na waandishi bora wa filamu nchini ambao kupitia
kazi zao watakuza kipato chao na pato la taifa kwa ujumla.
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amesisitiza kwamba
filamu ni uchumi, ni ajira na ndiyo maana serikali imeamua kuirasimisha
ambapo ameishukuru serikali kwa kufikisha mafunzo hayo hadi ngazi za
mikoani.
Zaidi
ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo
hayo ya filamu na maigizo kupitia Bodi ya Filamu nchini ambapo
wamefurahishwa nayo na kuahidi kuyatumia kuboresha kazi zao ikiwemo
kuzalisha filamu na vipindi vya luninga vyenye maudhui bora.
Tazama HAPA Mafunzo ya mkoani Mwanza











No comments :
Post a Comment