Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika
Kamtanda Hamisi akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi
wakati akitoa maoni yake baada ya Rais Dk.John Magufuli kuwaruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa. Habari na maelezo ya wafanyabiashara wengine soma habari hapo chini.
wakati akitoa maoni yake baada ya Rais Dk.John Magufuli kuwaruhusu wafanyabiashara kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa. Habari na maelezo ya wafanyabiashara wengine soma habari hapo chini.
Muuza mitumba Hassan Bakar.
Mfanyabiashara Juma Abdul
Mfanyabiashara wa viatu Evord Lyimo.
Mfanyabiashara wa matunda Salum Ramadhan.
Mfanyabiashara wa mitumba Salum Mwinyimkuu
Wauza
mitumba katika Soko la Tandika wakiwa wamepozi kwa furaha baada ya Rais
Dk.John Magufuli kuwaruhusu kufanya biashara zao pasipo kubugudhiwa.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYABIASHARA
ndogo ndogo wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamempongeza
Rais Dk.John Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanyabiashara zao bila
ya kubugudhiwa na kumtaja kuwa ni kiongozi wa wanyonge na watu wa chini.
Kauli hiyo wameitoa leo asubuhi wakati wakitoa maoni yao baada ya Rais kutoa tamko hilo Dar es Salaam jana.
Mchuuzi wa urembo katika Soko la Tandika Kamtanda Hamisi alimshukuru rais kwa kuwaruhusu na kuwajali watu wa chini.
“Nawaomba
wafanyabiashara wenzangu ruhusa ya rais isiwe kibali cha sisi kuanza
kupanga biashara zetu barabarani tufuate sheria” alisema Hamisi.
Muuza
mitumba Hassan Bakar alisema Rais Magufuli yupo vizuri tunakila sababu
ya kumpongeza katika jambo hilo la kuwatetea wanyonge yupo katika mstari
ulionyooka na tumeteseka kwa miaka mingi.
Juma Abdul alisema anafuraha kwa uamuzi huo wa rais kwani ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa uchaguzi mkuu.
“Tulitukanwa sana na kunyang’anywa bidhaa zetu sasa baba yetu Magufuli ametuona na kutuondoa kwenye mateso hayo” alisema Abdul.
Mfanyabiashara
wa viatu Evord Lyimo alisema walikuwa wakiishi kama digidigi na
kupoteza bidhaa zao baada ya kuchukuliwa na mgambo sasa vitendo hivyo
vimekoma kupitia kwa rais wetu tunampongeza kwa hatua hiyo.
Salum
Mwinyimkuu alisema Rais yupo sahihi kwa hatua hiyo, kazi hii
tunayoifanya ndio ajira yetu inayotuwezesha kuishi na familia zetu.
Mfanyabiashara
wa matunda Salum Ramadhan alisema wanamshukuru rais kwa ruhusa hiyo
hivyo akatoa mwito kwa wenzake kuzingatia sheria ya kutofanya biashara
barabarani na kuzuia vyombo vya moto visipite.
No comments :
Post a Comment