Daladala
zinazo fanya safari kati ya Tegeta Nyuki zikiwa zimesongamana katika
Kituo cha Daladala nje ya geti Kuu la Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam juzi baada ya kupangiwa na Mamlaka ya Usafiri wa
Nchikavu na Majini (SUMATRA) yawe yanashusha na kupakia hapo na
kusababisha adha kubwa ya abiria na madereva hao walitii nakuyapeleka
magari yao Muhimbili kama walivyo elekezwa na (SUMATRA) nakumfanya
Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi, Adnan Kondo kuwaamuru waondoke na warudi walikotoka
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter
Mashishanga (kulia) akizungumza jambo wakati walipofika katika Kituo cha
Mabasi cha Feri kwa lengo la kujionea changamoto mbalimbali
Mwenyekiti wa Daladala Zinazofanya Safari ya Tegeta Nyuki (Gosbart mushaka) akizungumza jambo wakati Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter
Mashishanga kufika katika Kituo cha Gerezani na Timu yake kujionea hali
halisi zilizopo kituoni hapo na aweze kujadiliana na viongozi mbalimbali
na kulipatia jawabu swala la Daladala za Tegeta Nyuki ambazo awali
zilikuwa zikipaki Kariakoo Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA KHAMISI
MUSSA)
Abiria wakishuka kwenye daladala
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter
Mashishanga (kulia) akizungumza jambo Dar es Salaam jana wakati
alipofanya ziara ya kutembelea baadhi ya vituo vya mabasi vya Muhimbili,
Feri na Gegerezani akiwa amwongozana na Viongazi mbalimbali wa SUMATRA,
Wamiliki wa Mabasi hayo, Madereva na Wenyeviti na makatibu hasa wanjia
ya Tageta kujionea hali halisi na changamoto ili waweze kuzitolea
majawabu
Ofisa
leseni na Udhibiti Usafiri wa barabara Mkoa wa Dar es Salaam, Bernard
akilipiga picha Gari Moja lilofika kwa majaribio katika Kituo cha
Mabasi cha Muhimbili
Kaimu Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala (katikati aliyevaa miwani) akizungumza jambo wakati wa Ziara ya
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter
Mashishanga kutembelea maeneo mbalimbali ya vituo iliwemo Kituo cha
Daladala cha Muhimbili ambapo alianzia hapo na kutembelea Feri na
Gerezani Dar es Salaam jana
Kituo cha daladala Gerezani
No comments :
Post a Comment