Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula (kulia) akikagua nyumba za
mradi wa makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
wilayani Mlele mkoani Katavi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda bibi
Lilian Matingana, katikati yao ni Meneja wa NHC mkoani KataviBw. George
Magembe.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa
Wilaya ya Mlele mara baada ya kusikiliza kero na matatizo yao kuhusu
sekta ya ardhi. Dkt. Mabula amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Katavi
na ameeleke amkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akitoa maelekezo
kwa karani wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya –Mpanda, namna bora ya
utunzaji kumbukumbu za majalada ya mashauri wakati alipotembelea Baraza
hilo ili kufuatilia utendaji kazi wake.
Meneja wa Shirika la Nyumba la
Taifa Mkoa wa Katavi Bw. George Magembe akitoa maelezo ya miradi
mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya makazi na biashara inayotekelezwa na
Shirika mkoani Katavi wilayani Mpanda kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (aliyesimama) akizungumza na
wananchi wa Kata ya Kazima katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
mkoani Katavi mara baada ya kusikiliza kero wanazokumbana nazo
wanapohitaji huduma za sekta ya ardhi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
Bibi Lilian Matinga na kulia kwa Dkt. Mabula ni Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw. Willy Mbogo.
Mkazi wa Kata ya Nsemulwa
katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Bibi
Maria akieleza tatizo alilo nalo kuhusu huduma za ardhi mbela ya Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula (kushoto) akizungumza na
wananchi wa Kata ya Nsemulwa mkoani Katavi mara baada ya kusikiliza
matatizo yao kuhusu huduma za sekta.
………………………..
Serikali imeagiza Halmashauri
zote nchini kutokuchua ardhi ya mtu bila ya kulipa fidia wakati wa
kutwaa maeneo kwa ajili ya mpango wa matumizi mbalimbali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi DKT. Angelina Mabula amesema hayo wakati wa ziara ya
kiazi mkoani Katavi wakati alipotembelea kwa lengo la kukagua utoaji
huduma za sekta ya ardhi unavyofanyika pamoja na kukagua shughuli
mbalimbali.
Amesema Serikali ilikwishatoa
maealekezo hayo ya kuzingatia Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 iliyofayiwa
mabadiliko baadaye ambayo inatoa haki ya mtu kulipwa fidia ya ardhi tupu
na maendelezo yake pindi ardhi yake inapotwaliwa.
“unapopima maeneo kulingana na
miji inavyokua mikubwa ama inavyotanuka, lazima kwanza fidia ilipwe kwa
mtu anayekutwa pale ndipo wapishe katika maeneo yao, na iwapo mtu huyo
analo eneo kubwa linalobaki pia alipwe fidia kwa mujibu wa
sharia,”alisema Dkt. Mabula.
Alisisitiza pia lazima kipaumbele
cha umilikishaji wa kiwanja kitolewe kwa mtu ambaye eneo lake
limechukuliwa badala ya kumilikisha watu wengine wenye uwezo waki fedha.
Amesema kwamba iwapo kutakuwa na
uhamishowa watu wakati wa utwaaji ardhi basi uwe ni kwa ajii ya kupisha
huduma za msingi za jamiik ama vile ujenzi wa shule, hospitali, barabara
ama Mahakama na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.
Naibu Waziri huyo wa Ardhi ataendelea na ziara yake ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Rukwa, Songwe na Mbeya
No comments :
Post a Comment