Friday, December 2, 2016

MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA KUONGOZA WANANCHI NA WAANDISHI WA HABARI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA MAATHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHURU

 picha wa kwanza  kushoto ni meneja  Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa kampuni ya Zara  Zainabu  Ansell wakati wa mkutano wao na waandisi wa habari juu ya   maandalizi ya miaka 55 ya uhuru ambayo yanatarajiwa kufanyika december 9
 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya  Zara Tours Zainabu Anselm  akiongea juu ya kampuni yake ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio vilivyopo ndani ya nchi yetu na sio kuendelea kuviona kwa mbali tu na kuvisikia
 Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi za taifa (Tanapa) Allen Kijazi akiongea na waandishi wa habari
meneja  Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  wa kwanza kushoto ni Afisa uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete
 
 Habari  Picha na Woinde Shizza,Arusha
Aliyekuwa mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa jenerali msataafu geogre waitara anatarajiwa kuongoza  msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya  uhuru wa tanzania,
Aidha katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii (ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha  watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
Alisema kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi mashuhuri  wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama Uhuru Epedition .
Kijazi alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.
“Katika maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa “aliongeza kijazi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani  wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.
Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.

No comments :

Post a Comment