Diwani wa kata ya Majohe
Bw.Waziri Mwanavyale akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada
wa shilingi milioni 10 toka kwa Shirika la Petroli Nchini (TPDC) kwa
ajili ya kujenga Ofisi ya Serikali ya Mtaa.Kulia kwake ni Kaimu
Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi
Kapulya Musomba na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Bi.Elizabeth Thomas akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa
shilingi milioni 10 toka kwa Shirika la Petroli Nchini(TPDC) kwa ajili
ya Ulinzi mzuri wa Bomba la Gesi linalopita jirani yao.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la
Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akizungumza
na wananchi wa Pugu Majohe kabla ya kuwakabidhi shilingi milioni 10 kwa
ajili ya kujenga Ofisi ya Serikali ya Mtaa.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la
Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akimkabidhi
hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Serikali ya
Mtaa,katikati ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas.
Wakazi wa Majohe ni wadau wa Bomba la Gesi linalotokea Mtwara hadi Dar
es Salaam.
Wakazi wa Pugu Majohe wakifurahi
kupatiwa hundi ya shilingi milioni 10 kutoka Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini (TPDC) kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa .
Wakazi wa Majohe ni wadau wa Bomba la Gesi linalotokea mtwara hadi Dar
es Salaam.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
…………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli
Nchini (TPDC) limeipatia shilingi milioni 10 Ofisi ya Serikali ya Mtaa
wa mji Mpya iliyopo Pugu Majohe Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo leo
Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Shirikahilo, Mhandisi Kapulya
Musomba alisema wakazi wa Pugu-Majohe wameamua kutoa fedha hizo kutokana
na wakazi wa eneo hilo kupitiwa na bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam.
“TPDC hatuwezi kulinda bomba hili
la Gesi kila mahali linapopita, wadau hawa wamekuwa ni sehemu ya
kulinda bomba hili wanalinda pia uchumi wa nchi kwa sababu gesi hii pia
inatumika kuzalisha umeme wa viwanda” Alisema Musomba.
Aidha Mhandisi Musomba ametoa
wito kwa wananchi wa Pugu Majohe kuacha kuchimba mchanga karibu na
bomba hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaharibu miundombinu ya
bomba hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas ameishukuru TPDC kwa kuwawezesha
kupata kiasi hicho kwani kitawasaidia katika ujenzi wa Ofisi hizo na pia
katika maendeleo ya Pugu Majohe na kuwaomba kuendelea kusaidia katika
maeneo tofauti ya Wilaya ya Ilala.
Nae Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa mji Mpya-Majohe Bw.Geofrey Chacha amesema kuwa wamejiskia faraja
sana kwa kupata msaada huo kutoka TPDC kwani utaweza kusaidia kumalizia
ujenzi wa Ofisi zao.
Mchango huu umetupa nguvu katika
kuwahamasisha wananchi katika eneo hili kuweza kuwa walinzi wazuri wa
miundombinu hii ambayo inagusa maslahi ya Taifa letu” alisema Chacha.
No comments :
Post a Comment