Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na
Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakijadili masuala pamoja na
wakurugenzi wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF, Profesa
Godius Kahyarara na Bw.William Erio pamoja na Mbunge Jimbo
la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) kuhusiana na mradi
mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la
Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni uwekezaji wa pamoja wa mifuko
hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi
huo mwishoni mwa wiki.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango,
Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara inayoelekea sehemu ya
mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA
JKT.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri wa
Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo
kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi
mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la
Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni uwezeshaji wa pamoja wa mifuko
hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi
huo mwishoni mwa wiki.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na
Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakimsikiliza Mbunge Jimbo
la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) ambae jimboni kwake
ndipo unatekelezwa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Wananchi wa kijiji cha Kidunda,
kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo
muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya
100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo
jirani na mradi.
Wananchi wa kijiji cha Kidunda,
kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo
muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya
100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo
jirani na mradi.
Wananchi wa kijiji cha Kidunda,
kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo
muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya
100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo
jirani na mradi.
Washirika muhimu! Wakurugenzi
wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF, Profesa
Godius Kahyarara (kulia) na Bw.William Erio (kushoto) wakisikiliza
hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,
Jenister Mhagama alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni mwa wiki.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati
alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki ambapo aliwahakikishia wakazo
hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi
utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa pili kulia) na Waziri wa
Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (wa tatu kulia) walipotembelea bwawa
la Kidunda lililopo kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya
Morogoro Vijijini. Mawaziri hao walipokea ombi la kuwezesha ujenzi wa
daraja litakalounganisha kijiji hicho na Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa
Pwani ili kurahisisha mawasiliano baina ya mikoa hiyo miwili.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na
Mpango, Dr. Phillip Mpango (kulia) wakijipongeza baada ya kukamilisha
ziara hiyo muhimu. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko hifadhi ya jamii
wa NSSF Profesa Godius Kahyarara.
Waziri wa Fedha na Mpango, Dr.
Phillip Mpango (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa
mfuko hifadhi ya jamii wa PPF Bw.William Erio
……………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu,
MIFUKO ya hifadhi ya jamii
ya NSSF na PPF imeanza utekelezaji wa awali wa mradi mkubwa wa ujenzi wa
kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani
Morogoro...
ikiwa ni jitahada ya mifuko hiyo kwa pamoja kuunga mkono
muelekeo wa serikali ya awamu ya tano wa kuwekeza kwenye uchumi wa
viwanda.
Kukamilika kwa kiwanda hicho
kinachotajwa kuwa kitakuwa ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki, kutaongeza
uzalishaji wa sukari wa hapa nchini ambapo zaidi ya tani laki mbili
(200,000) zitakuwa zikizalishwa kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi
ya 100,000 kwa hatua ya awali.
Akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati
alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki, Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama aliekuwa ameambatana na
Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango, mbali na kuipongeza
mifuko hiyo, aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa
mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi
wa eneo hilo hususani vijana.
“Mradi huu una ushawishi mkubwa
kutoka kwa Rais John Magufuli kutokana na adhma yake ya kuibadili
Tanzania kuwa nchi ya viwanda na umekuja kwa wakati muafaka. Nataka huu
uwe wa mfano,’’ alisema Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Mkuu wa
mkoa wa Morogoro Dk Stephen Kebwe, Mbunge Jimbo
la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba pamoja na wawakilishi wa
kampuni ya Mkulazi Holding inayosimamia utekelezaji wa mradi huo pamoja
na viongozi wengine wa serikali.
Waziri Mhagama aliwaomba
watekelezaji wa mradi huo kuainisha mapema aina ya rasilimali watu
watakaohitajika kwenye mradi ili waanze kuandaliwa mapema kuepuka suala
la kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchi kuja kufanya kazi ambazo
zingeweza kufanywa na wataalamu wa ndani iwapo wangeandaliwa mapema.
Kwa upande wake Waziri Mpango
alisema tayari serikali imeshatenga sh bilioni 17 katika mwaka wa fedha
2016/2017 kwa ajili ya kumalizia fidia na mipaka kwa wakazi wanaoishi
kwenye shamba la miwa kwa ajili ya kiwanda hicho lenye ukubwa wa ekari
63,000.
“Lengo kubwa hapa ni kuzalisha
sukari itakayotuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani na kuuza nje ya
nchi pamoja na bidhaa ambatano ikiwemo ethanol. Pia nitoe wito kwa
vijana wa eneo hili kuhakikisha wanakuwa katika vikundi ambavyo
vitawawezesha kutekeleza kwa urahisi miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha
mashamba yatakayosaidia kuongeza malighafi kwa kiwanda hiki,’’ alisema.
Zaidi Dk. Mpango aliwataka
viongozi wa serikali wilayani humo wakiwemo wahandisi kuhakikisha
wanatoka maofisini ili kukagua ujenzi wa miundombinu inayoambatana na
mradi huo ikiwemo barabara inayojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT
kuelekea eneo la mradi.
“Ile barabara ndio itatumika
kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka na kuelekea kiwandani na iwapo
itatengenezwa chini ya kiwango kutokana na uzembe tu wa kushindwa
kumsimamia mkandarasi hatutaelewana,’’ alisema Dk Mpango huku akiionya
kampuni ya SUMA JKT kutekeleza mradi huo kwa viwango vya ubora ili
kulinda imani ya serikali kwa makampuni ya umma katika utekelezaji wa
miradi yake mbalimbali.
Kwa upande wake Dr Kebwe mbali na
kuahidi kuusimamia vema mradi huo hadi kukamilika kwake, alitoa wito
kwa vijana wa eneo hilo kuhakikisha wanafanya kazi badala ya
kuwategemea zaidi wakina mama na wazee kwenye shughuli za uzalishaji.
“Ninazo takwimu zinazoonyesha
kuwa katika kata hii wakina mama na wazee ndio wanaofanya kazi zaidi
kuliko vijana na kwa mujibu wa takwimu hizo wakina mama na wazee
wanafanya kazi kwa asilimia 68 huku vijana mpo…mbadilike!,’’ alionya.
No comments :
Post a Comment