Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya
afya pamoja na ukatili wa kijinsia kwa vijana na wanawake nchini la
Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii
leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na
mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya
shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.
#BMGHabari
Wadau
wa afya mkoani Mwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la
TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, wakati akizungumza kwenye mkutano
wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika
utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi
mkoani Mwanza.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo
wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na
mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya
shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.
Mratibu
wa Afya ya Uzazi ngazi ya jamii mkoani Mwanza, Esperance Makuza,
akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi ngazi ya mkoa wa
Mwanza.
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, akifafanua namna mradi huo ulivyofanya kazi, mafanikio na changamoto zake.
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, akifafanua namna mradi huo ulivyofanya kazi, mafanikio na changamoto zake.
Baadhi ya wadau wa afya mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano wa kushirikishana
uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya
pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi
Baadhi ya wanahabari pamoja na wadau wa afya mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano wa kushirikishana
uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya
pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi
Mmoja wa watumishi wa afya mkoani Mwanza
Mradi
huo ulifadhiriwa na Pink Ribbon Red Ribbon pamoja na washirika wengine
kama wanavyoonekana katika picha. Mitandao ya simu ilisaidia kutoa
nambari za bure ambazo ni 117 kwa ajili ya wananchi kupiga ili
kuelimishwa kuhusu Saratani.
Uelewa
kuhusu dalili za awali za maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi
kwa wanawake mkoani Mwanza, umeongezeka na hivyo kufanya idadi ya
wanawake wanaojitokeza kupima maambukizi hayo kufikia wanawake 60 kwa
mwezi.
Hatua
hiyo imefikiwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali kupitia
wizara ya afya kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ikiwemo TAYOA
katika kuhakikisha akina mama nchini wanafahamu umuhimu wa kufanya
uchunguzi wa awali kuhusu maambukizi ya saratani kwa ujumla.
Hayo
yamebainishwa Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Shirika la TAYOA,
Elizaberth Ndakidemi, kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu,
changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya
mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na
shirika hilo.
Katika
mradi huo ulioanza kutekelezwa mwezi April mwaka 2014, zaidi ya akina
mama elfu 20 mkoani Mwanza wamefikiwa na kupewa elimu kuhusiana na
saratani ya shingo ya kizazi, kuwaongezea ujuzi watoa huduma za afya
wapatao 70 katika ngazi za jamii pamoja na kusaidia upatikanaji wa vifaa
vya uchunguzi wa dalili za awali za saratani hiyo katika vituo vya afya
mkoani Mwanza ambapo tamati ya mradi huo ni Disemba 31 mwaka huu.
Aidha
mradi huo umesaidia kuwasafirisha akinamama 392 mkoani Mwanza, kwenda
katika hospitali za rufaa ikiwemo Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi
wa Saratani ya shingo ya kizazi ambapo miongoni mwao zaidi ya akina mama
70 wamepatiwa matibabu.
Awali
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, amebainisha kwamba
wakati mradi huo unaanza kulikuwa na dhana potofu kuhusiana na ugonjwa
wa saratani ya shingo ya kizazi ambayo wanawake wengi walikuwa wakiamini
wamerogwa na hivyo kuchelewa kufika hospitalini huku baadhi yao
wakikimbiwa na waume zao.
Akizungumza
kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi mkoani Mwanza, Mratibu wa Afya ya
Uzazi ngazi ya jamii, Esperance Makuza, amewahimiza watoa huduma wa
afya walionufaika na mafunzo yaliyotolewa katika mradi huo, kuyatumia
mafunzo hayo kutoa huduma zinayostahili ili kuwanusuru akina mama na
madhara yatokanayo na saratani hiyo.
Inaelezwa
kwamba zaidi ya asilimia 80 ya akina mama wanaougua saratani ya shingo
ya kizazi nchini hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kufanya uchunguzi
na kupatiwa tiba mapema, ikizingatiwa kwamba saratani hiyo hutibiwa
ikiwa mgonjwa atawahi matibabu.
Aidha
akina mama wanakumbushwa kuzingatia kanuni bora za kiafya ikiwemo
kufanya mazoezi, kujiepusha na uvutaji wa sigara, ulevi pamoja na
wapenzi wengi ili kuondokana na maambukizi ya saratani ya shingo ya
kizazi.
No comments :
Post a Comment