Wednesday, December 21, 2016


mema
Mbunge wa
Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mkewe Neema baada ya
mahakama kumalizika leo.Picha na Vero Ignatus
Blog.
 Na.Vero Ignatus,Arusha
 
 
Jaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya
Arusha Dkt.Modesta Opiyo  amewapa siku kumi(10)mawakili wa mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema wawe wamewasilisha notisi ya kukata
rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya chini iliyomnyima dhamana Lema

.



Agizo
hilo limekuja kutokana na mahamama kutoridhishwa na hoja za maombi ya
mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali
dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa
mbunge hu



Jaji
Dkt.Modesta Opiyo  mahakama kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi
yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi
walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa
mahakamani,ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa
lazima.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema
,Shekh
Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi
kuanzia leo,hadi hapo tar 30dec2016 shauri hilo litakaposikilizwa
tena.
                                                     

Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya
uchochezi aliyosomewa katika
mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha
Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya
kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka
huu Mkoani
Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara
katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais
Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi
kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.

No comments :

Post a Comment