Kaimu Meneja Mkuu Kampuni ya
Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka akizungumza
na wataalamu wa nishati ya jotoardhi kutoka TGDC, Shirika la Msaada wa
Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) na Chama cha
Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya
kuwajengea uwezo wataalamu wa jotoardhi nchini.
Mtaalamu wa Nishati kutoka Shirika
la Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) Dkt.
Thrainn Fridrikson akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa
nishati ya jotoardhi nchini, mafunzo hayo yamedhaminiwa na ESMAP na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Banki ya Dunia Tanzania.
Wataalamu wa nishati ya jotoardhi
kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Shirika la
Msaada wa Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) na Chama
cha Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) katika majadiliano wakati wa mafunzo
maalum ya kuwajengea uwezo yaliyafanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Benki ya Dunia Tanzania.
Mtaalamu kutoka Chama cha
Kimataifa cha Jotoardhi (IGA) Mhandisi Cristian Scanzoni akiwasilisha
mada kuhusu usimamizi wa uchorongaji visima vya jotoardhi wakati wa
miradi. Mafunzo hayo maalum yalifadhiliwa na ESMAP na yalilenga
kuwajengea uwezo wataalamu wa Jotoardhi Tanzania Shirika la Msaada wa
Usimamizi wa Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) laipongeza TGDC
Picha Na: Johary Kachwamba – TGDC.
……………………….
Na. Johary Kachwamba – TGDC
Shirika la Msaada wa Usimamizi wa
Nishati chini ya Benki ya Dunia (ESMAP) laipongeza Taasisi ya nishati ya
joto ardhi nchini (TGDC) kwa jitihada walizofikia na kuahidi kuendeleza
ushirikiano nao.
Pongezi hizo zimetolewa na
Mtaalamu wa Nishati kutoka Shirika la Msaada wa Usimamizi wa Nishati
chini ya Benki ya Dunia Dkt. Thrainn Fridrikson wakati wa semina ya
kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati ya joto ardhi nchini iliyoendeshwa
na wataalamu kutoka Chama cha Kimataifa cha Joto ardhi (International
Geothermal Association – IGA) mapema wiki hii.
‘Nina imani kubwa na uelewa
mlionyesha katika semina hii kuwa mtakuwa mmepata elimu yakutosha
itakayowasaidia katika uvumbuzi wa nishati hii ya joto ardhi lakini pia
mafunzo haya yatasaidia kurahisisha shughuli zenu na kupelekea
uzalishaji wa nishati hii kuanza mapema hapanchini, alisema Dkt.
Fridrikson.
Akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo hayo, Kaimu Meneja Mkuu (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka alitoa
shukrani kwa ESMAP na kusema ni fursa muhimu kwa TGDC kama kampuni
katika maandalizi ya kuendeleza nishati ya jotoardhi inayolenga kusaidia
taifa kufikia malengo yaliyo katika dira ya 2025.
Kwa upande wake Mhandisi
Uchorongaji, Amani Christopher kutoka (TGDC) alisema kuwa mafunzo
yamewaongezea utaalamu katika utekelezaji wa kazi zao za kitafiti na
wanatarajia kufanya kazi kwa wepesi zaidi tofauti na awali kwani mafanzo
hayo yamewaongezea uelewa katika sekta hiyo.
Mafuzo hayo ya siku nne
yalijikita katika kuwajengea uwezo wahandisi wa uchorongaji, pamoja na
sekta nyingine kama usimamizi manunuzi, taratibu za kisheria, na
Usimamizi wa fedha za kugharamia miradi.
Mwisho
No comments :
Post a Comment