Friday, December 2, 2016

NEC yakutana na ugeni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani

nec
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) kushoto.Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura, Mhandisi Manyiri Isack na Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia Adolf Kinyero.Ujumbe huo umekuja kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) na kutambulisha Teknolojia mpya ya mashine ya Kuandikisha Wapiga Kura.
nec-1
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni wa Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB), Lee Ju-Hwan  (katikati) akimueleza jambo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani wakati walipotembelea Ofisi za NEC jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mtafiti wa chama hicho, Moon Jueun.
nec-2
Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura, Mhandisi Manyiri Isack (kushoto) akimuonesha Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (katikati) kamera kwenye mashine ya kuandikisha wapiga kura wakati ujumbe kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) ulipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kulia ni Mtafiti wa chama hicho, Moon Jueun, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni, Lee Ju-Hwan, Mtaalamu wa Uchaguzi Park jae Sung kutoka AWEB
nec-3
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akiweka kidole kwenye mashine ya kuandikisha Wapiga kura huku Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia Adolf Kinyero akishuhudia. Kulia ni Mtafiti wa Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB), Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park jae Sung (aliyevaa miwani).
nec-4Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (aliyeshika mashine ya kusajili wapiga kura) akieleza utendaji kazi wa mashine hiyo kwa baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) (kulia).
nec-5Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Adolf Kinyero (kulia) akimuonesha Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (katikati) na Mtafiti wa Chama hicho, Moon Jueun, jinsi BVR inavyofanya kazi.
nec-6
Mtaalamu wa Uchaguzi kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB) Park jae Sung (katikati) akiwaeleza baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kifaa kinachotumia Teknolojia ya Kuandikisha wapiga Kura.
nec-7
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka Chama cha Bodi za Uchaguzi Duniani (AWEB).Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mipango na Operesheni, Lee Ju-Hwan, Mtafiti, Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi, Park jae Sung.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura, Mhandisi Manyiri Isack na Mkuu wa Sehemu ya Kanzidata ya Daftari na Mifumo ya Kijiografia, Adolf Kinyero.
nec-9Mashine inayotumika kuandikisha Wapiga kura inayotumia Teknolojia ya Kisasa ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejifunza jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
Picha na Hussein Makame, NEC.
………………………….
Christina Njovu, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imepokea ujumbe Taasisiya  Tume za Uchaguzi Duniani(AWEB) uliokujakujifunza na kubadilishana uzoefu katika masualambalimbali ya uendeshaji Uchaguzi.
Ujumbe huoumekujakujifunza kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) juu ya masualambalimbali ya uendeshaji Uchaguzi nchiniikiwemomatumizi ya vifaa vya kuandikishiawapigakura.
Mkurugenzi wa Mipango na OparesheniBw. Lee Ju-Hwan  alisema kuwa yeye na ujumbe wake wamekujakubadilishana uzoefu katika technolojiaya Kuandikisha Wapiga Kura.
Ujumbe huoumekutanana Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzonayeofisinikwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo kutembeleaofisimbalimbali za Tume hiyo na kujifunza.
Wakiwa katika kikao na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ujumbe huo wa watu watatuulijifunza namna mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) inavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyowezakuandikisha Wapiga Kura wengi kwa kutumiamashinetechnolojiahiyo  nachangamoto zake.
Aidha ujumbe huoumekuja na aina mpya yatechnologia ambayo inauwezo wa kuandikisha Wapiga Kura, kutuma taarifa za Wapiga katika kanzidata kutoka katika kituo cha kujiandikishia na  kuhakiki Wapiga Kura siku ya Uchaguzi .
Mashine hiyo ambayo nindogoukilinganisha na ile BVR inauwezo wa kutumiwa na mtummojaambayeatawezakumuandikisha Mpiga Kura katika hatua zote hadi kupata kitambulisho cha mpiga Kura na inabebeka kirahisi.
Ujumbe huoumeongozwana Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park Jae Sumg.
Technologiahiyo mpyainawezakurahisishautendaji kazi katika masuala ya uandikishajiwapiga Kura, kuhakikiwapigakura na kutuma taarifa katika kanzidara.

No comments :

Post a Comment