Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo
Business Agency, Bi Ubwa Ibrahim akihutubia wakati wa uzinduzi wa kugawa
miradi ya sungura kwa wajasiriamali eneo la Majohe, Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo
Business Agency, Bi Ubwa Ibrahim akielezea jinsi mradi wa sungura
utakavyowanufaisha wanachama wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa
kugawa miradi ya sungura kwa vikundi vya wajasiriamali eneo la Majohe,
Dar es Salaa. Anayesikiliza kushoto ni Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora,
Donald Bombo. Jumla ya sungura 600 waligawiwa kwa wanachama wa Namaingo.
Azingumza kwa niaba ya Serikali,
Mkurugenzi huyo kutoka Ofisi ya Rais, Bombo alimpongeza Bi Ubwa kwa
ujasiri na uthubutu alionao wa kuanzisha miradi mbalimba inayosaidia
kuwanufaisha wananchi na kuinua vipato vyao. Aliahidi kuwa serikali
itakuwa bega kwa bega naye kuhakikisha mipango ya kusaidia kiuchumi
wananchi inafanikiwa.(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO
BLOG)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Rabbit Republic
mwanzilishi wa ufugaji wa sungura kutoka Kenya, Moses Mutua akielezea
mipango yake ya kuzanzisha machinjio makubwa ya kisasa ya sungura hapa
nchini.Jana vikundi 20 vya wajasiriamali viligawiwaq sungura ambapo kila
kikundi kilipata sungura 27 wa kike na madume matatu.
Mutua akionesha sungura wa mradi ambao
ameiuzia Kampuni ya Namaingo kwa ajili ya miradi ya wajasiriamali. Nyama
ya sungura itakuwa inauzwa nje ya nchi ambapo kila siku itauzwa tani 2.
Bi Ubwa akiwa na mmoja wa wanachama wakicheza muziki kwa furaha wakati wa hafla hiyo
Msanii akitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji sungura
Baadhi ya wajasiramali wakicheza muziki
Wajasiriamali wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa Namaingo akihutubia
Mmoja wa viongozi kutokaOfisi za Namaingo mikoani akitoa ushuhuda wa miradi waliyonayo na wanayotarajia kuianzisha.
Sehemu ya magari ya wajasiriamali waliofika katika uzinduzi wa miradi ya wajasiriamali
No comments :
Post a Comment