Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na
wananchi wa Kijiji cha Kishuro,Kata ya Ngenge Wilaya ya Muleba, Mkoa wa
Kagera. Dkt.Kalemani amefanya ziara Wilayani humo ya kukagua Mradi
utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili na kueleza mipango ya Serikali
kutekeleza Awamu ya Tatu ya mradi husika.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na
wananchi wa Kata ya Ngwanseri,wilaya ya Muleba, wakati wa ziara yake ya
kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard
Ruyango,akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt.Medard Kalema ni kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu
ya Pili.Wengine katika picha ni baadhi ya Viongozi wa Halmashauri
hiyo,Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na
Wakandarasi wanaotekeleza mradi husika.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt.Medard Kalemani, (Wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mbunge
wa Jimbo la Muleba Kusini, Prof.Anna Tibaijuka (wa pili kushoto),Mkuu
wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango,(wan ne kushoto)pmoja na
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na Wakandarasi
wanaotekeleza mradi wa REA Awamu ya Pili.
Mmoja wa Wananchi katika akiuliza jambo
wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard
Kalemani(hayupo pichani) katika Kata ya Ngwanseri.
Wananchi wa Kata za Ngwanseri na Ngenge
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani na
ujumbe wake wakati wa ziara yake a kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA
Awamu ya Pili wilayani Muleba.
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof.Anna
Tibaijuka (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati na
Madini,Dkt.Medard Kalemani ( katikati) mara baada ya kumaliza mkutano
wake na wananchi wa Kijiji cha Kishuro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Muleba Mhandisi Richard Ruyango.
Wananchi wa Kijiji cha Kishuro Wilaya ya
Muleba, wakisoma Jarida la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani
(hayupo pichani) akieleza utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili na
mipango ya Serikali ya kutekelza REA Awamu ya Tatu.
……………..
Na Asteria Muhozya, Muleba
Imeelezwa kuwa, Serikali imepanga kutumia
Nguzo za Zege katika utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu, unaotarajia kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi
Januari, 2017 chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana
na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati wa ziara
yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA Awamu ya Pili katika Kata
za Ngenge na Ngwanseri, Wilayani Muleba Mkoani Kagera, pamoja na kueleza
mipango ya Serikali katika utekelezaji wa mradi husika Awamu ya Tatu.
Dkt. Kalemani amesema kuwa, lengo la
kutumia nguzo hizo za zege ni kutokana na uimara wake utakaowezesha
upatikanaji umeme wa uhakika na kuepuka kuchomwa na kuongeza kuwa,
tayari nguzo hizo zimeanza kutumika katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumzia utekelezaji wa REA Awamu ya
Pili, amesema Serikali imetekeleza mradi huo kwa kasi kubwa kutokana na
dhamira yake ya kuhakikisha kuwa, ifikapo mwaka 2025 asilimia 75 ya
Watanzania wawe wameunganishwa na nishati hiyo ambayo ni kichocheo cha
shughuli za kiuchumi.
“ REA awamu ya pili imekamilika kwa
kiwango kikubwa. Vipo baadhi ya vijiji havijafikiwa kutokana na dosari
ndogo ndogo lakini tutavikamilisha kuwezesha utekelezaji wa Awamu ya
Tatu. Hata katika Wilaya hii vipo na tayari nimemwelekeza Mkandarasi
kukamilisha kazi hiyo haraka,”amesisitiza Dkt. Kalemani.
Akielezea mipango kwa Awamu ya Tatu,
amesema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kuwa, awamu hiyo inavifikia
vijiji vyote ambavyo havikuunganishwa katika Awamu ya Pili, visiwa
vyote, Taasisi mbalimbali, Sehemu zinazotoa Huduma za Kijamii zikiwemo
za Afya, shule na visima vya maji.
Aidha, alisema kuwa, kukamilika kwa
utekelezaji wa Miradi Ujenzi wa njia za Kusafirisha umeme wa Msongo
Mkubwa wa kV 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na
Singida kutawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika pamoja na kuchochea
uchumi wa viwanda hususan katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Wakati huo huo, Dkt. Kalemani ametumia
fursa hiyo kuzitaka Halmashauri zote nchini kushirikiana na TANESCO
kuweka utaratibu shirikishi ambao utawawezesha wananchi kupata huduma za
kuunganishiwa nishati hiyo kupitia utaratibu wa kuanzisha madawati ya
TANESCO katika maeneo yatakayotambuliwa ili kuwawezesha wananchi kupata
huduma hiyo kwa urahisi.
“TANESCO na Halmashauri, pangeni namna ya
kuwawezesha wananchi kufikiwa kwa urahisi na huduma za kunganishwa
nishati ya umeme. Mkubaliane kupanga siku maalum ambayo wananchi
watahudumiwa. Serikali inataka kila mwananchi apate umeme, hivyo tuweke
utaratibu ambao utarahisisha na kuwezesha azma hiyo kufikiwa kwa
haraka,” amesisitiza Dkt. Kalemani.
Pia, Dkt. Kalemani amewataka Wakandarasi
wote wakati wa utekelezaji wa miradi ya Awamu ya Tatu kuhakikisha kuwa,
wanajitambulisha katika Halmashauri na Mamlaka nyingine ili waweze
kutambulika ili kuepusha udanganyifu.
Vilevile, Dkt. Kalemani ameitaka TANESCO
kuwaidhinisha Wakandarasi wote watakaofanya kazi ya ‘wiring’ katika
nyumba za wananchi katika utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu ikiwemo kutoa
orodha zao ili kuwapunguzia wananchi kero ikiwemo kuwaepusha na utapeli
unaofanywa na baadhi ya wasiowaaminifu.
Akizungumzia Sekta ya Madini, Dkt.
Kalemani amewahamasisha wachimbaji wadogo wadogo kujiunga katika
vikundi ikiwemo kujisajiri katika Ofisi za Madini zilizopo katika
maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwawezesha wachimbaji hao kuomba
ruzuku kupitia vikundi pindi zinapotolewa na Serikali.
Katika ziara ya kutembelea Kata hizo, Dkt.
Kalemani ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard
Ruyango, Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA, TANESCO na
Wakandar
No comments :
Post a Comment