Mbunge wa jimbo la Kilolo Venance
Mwamoto wa tatu kulia akiongozana na kamati yake ya mfuko wa
jimbo kukagua miradi ya kimaendeleo na kuchangia miradi hiyo
pichani ni jengo la maabara ambalo limekwama kuendelea katika shule
ya Sekodari Ipeta
|
Mbunge Mwamoto akitazama shughuli za ujenzi wa vyoo katika shule ya Msingi Iramba |
|
Mbunge wa kilolo
Venance Mwamoto akikagua ujenzi wa choo cha wanafunzi shule ya
Msingi Iramba jana wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbali
mbali jimboni humo |
|
Mwamoto akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Ukumbi |
|
Shimo la choo shule ya Sekondari Ipeta |
|
Vyumba vya madarasa shule ya msingi Italula |
|
Vyoo vya zamani vya wanafunzi shule ya Msingi Kidabaga |
|
Ujenzi wa vyoo vya kisasa shule ya Msingi Kidabaga ukiendelea |
|
Majengo ya shule ya Msingi Kidabaga |
|
Nyumba ya mwalimu Kidabaga shule ya Msingi |
|
Maabara ya shule ya sekondari Ipeta ikiwa imesimama ujenzi wake |
|
Choo cha mwalimu mkuu shule ya Msingi Mdeke Kilolo
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto amechangia zaidi
ya Tsh milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbaali mbali ya
kimaendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi ,madarasa
,nyumba za walimu na Zahanati katika jimboni hilo huku akiwataka
viongozi wa serikali za vijiji na kata kuhakikisha wanakamilisha
ujenzi huo kwa wakati na ubora .
Pamoja
na kuwataka viongozi hao kusimamia ujenzi huo amesema atachukua
hatua kali kwa kiongozi yeyote wa serikali ya kijiji ama kata
ambaye atatafuna fedha hizo za ukamilishaji wa miradi hiyo ya
kimaendeleo jimboni humo.
Mbunge
huyo aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ukaguzi wa
miradi 9 inayoendelea kwa nguvu za wananchi na Halmashauri ya
wilaya ya Kilolo na kueleza kuvutiwa na miradi hiyo japo
kunahitajika msukumo wa haraka katika umaliziaji wa miradi hiyo
hasa ile ya vyoo vya wanafunzi ili kuwawezesha wanafunzi hao pindi
shule zinapofunguliwa kuwa na vyoo bora.
Alisema
kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kwa mvua kuchelewa kunyesha
katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Kilolo tofauti na miaka
mingine ameona ni vema kuwapunguzia makali ya michango wananchi
wake na badala yake sehemu ya michango ambayo walipaswa
kuchangia ili kukamilisha miradi hiyo kuibeba yeye kupitia mfuko
wa jimbo kwa kuchangia fedha hizo.
Kwani
alisema ni rahisi kwa wananchi kuchangia nguvu zao kwa
kushirikia katika ujenzi huo wa miradi hiyo kuliko kushiriki
kutoa fedha jambo ambalo kwa wananchi hao ni sawa na kuwatesa
kutokana na wengi wao waliuwa wakiishi kwa kutegemea kilimo na
hadi sasa matumaini ya kupata fedha kwa njia ya kilimo yametoweka
baada ya mvua kushindwa kunyesha .
“Ninawaombeni
sana wananchi wangu kwa sasa ninyi mshiriki zaidi katika
maendeleo kwa kuchangia nguvu zenu na mimi niwaunge mkono kwa
kuchangia fedha ili kuifanya miradi hii ikamilike kwa wakati”
Hata
hivyo alisema kuna baadhi ya maeneo wananchi wanachangamoto kubwa
ya barabara hasa zile zilizopo chini ya Halmashauri kuwa
barabara hizo zitafanyiwa matengenezo na ile ya Tanrod kutoka makao
makuu ya wilaya ya Kilolo hadi Ndiwili mpakani mwa jimbo la
Kalenga inaanza kujengwa kwa kiwango cha lami mapema mwakani na
kuwa kuanzia January ujenzi huo utaanza kwani barabara hiyo ipo
katika ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mbunge
Mwamoto alisema kuwa kwa suala la ujenzi wa Zahanati na vituo vya
afya wananchi wamejitahidi kwa maeneo mbali mbali aliyopita kukagua
ujenzi umefikia hatua nzuri na kutolea mfano ujenzi wa Zahanati
ya Masege ambao jengo lake bado kuezekwa na nyumba ya mganga
ipo katika hatua ya kuanza kupandisha kuta kuwa kukamilika kwa
Zanahati hiyo kutawawezesha wananchi hao ambao walikuwa
wakilazimika kufuata matibabu Kibengu na Usokami wilaya ya Mufindi
wataweza kutibiwa katika Zanahati hiyo.
Alisema
katika ziara yake hiyo aliyoambatana na wajumbe wa mfuko wa jimbo
kupitia fedha za mfuko wa jimbo Kijiji cha Mdeke ambako kuna
ujenzi wa vyoo vya wanafunzi amechangia Tsh milioni 1 na kwenye
ujenzi wa nyumba ya mwalimu amechangia Tsh milioni 2 , sekondari
ya Ipeta kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi amechangia
Tsh milioni 2, shule ya Msingi Kidabaga amechangia Tsh milioni 3 kwa
ajili ya vyoo na nyumba ya mwalimu ,Wangama amechangia Tsh milioni 1
kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ,Kitongoji cha Ifiga amechangia
Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuanzisha mkondo B wakati ujenzi wa
Zahanati na nyumba ya Mganga Masege amechangia Tsh milioni 5
Mbunge
Mwamoto alisema ujenzi wa kituo cha Afya Ukumbi amechangia Tsh
milioni 2 na katika ujenzi huo nguvu za wananchi ni Tsh milioni 35
na Halmashauri ni Tsh milioni 10 huku ujenzi wa vyumba
vyamadarasa shule ya Msingi Italula amechangia Tsh milioni 2 hata
hivyo alisema atafanya ziara ya ukaguzi na uchangiaji wa miradi
ya maendeleo katika jimbo zima ili kupitia mfuko huo wa jimbo
miradi yote iweze kupata mgao huo. |
No comments :
Post a Comment