Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi
Mshauri wa Kampuni ya H.P Gauff, Eng. Kini C. Kuyonza (wa tatu kulia),
inayosimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM
88.8. wakati alipokagua barabara hiyo, wilayani Babati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na mmoja wa madereva wa
Basi linalofanya safari zake katika mikoa ya Dodoma-Babati, wakati
alipokagua ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8.
Ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga
yenye urefu wa KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami ukiendelea.
Mradi huo unajengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s China Railway
Seventh Group na unatajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akishindilia nondo kwenye moja ya
ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8, inayojengwa kwa
kiwango cha lami, alipokuwa akikagua mradi huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikaza nondo katika ujenzi wa
barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8, alipokuwa akikagua
barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akishiriki kucheza ngoma za asili
ya Kirangi katika kijiji cha Bicha, wilaya ya Kondoa mara baada ya
kuongea na wakazi hao katika ziara yake ya ukaguzi wa mradi wa barabara
ya Dodoma-Babati.
Muonekano wa Daraja la Kelema
ambalo ni moja ya madaraja makubwa 4 yanayojengwa katika barabara ya
Mayamaya-Mela KM 99.35. Daraja hilo lenye urefu wa mita 205, lina uwezo
wa kubeba tani 100.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikagua tabaka la lami katika
barabara ya Mayamaya-Meya KM 99.35, alipokagua barabara hiyo.
……………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewatahadharisha watanzania kuepuka
vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya barabara husasan katika kipindi
hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Ameyasema hayo wakati akikagua
mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati yenye urefu wa KM 188.1,
sehemu ya Mela-bonga ambapo imeripotiwa kuwepo vitendo vya uharibifu wa
miundombinu kwa muda mrefu.
‘Napenda kutoa wito kwa watanzania
kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuacha vitendo vya kuchoma
matairi barabarani, kwani hali hii hupelekea kuharibu barabara kwa kiasi
kikubwa ambazo Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuzijenga”,
amesema Prof.Mbarawa.
Aidha, amekemea vitendo vya baadhi
ya madereva kumwaga mafuta barabarani na baadhi ya wananchi kupitisha
mifugo kwenye barabara ambapo vyote kwa pamoja vinaharibu miundombinu ya
barabara.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwemo kuwaripoti wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara nchini.
Sambamba na hilo, amewaasa
madereva wa vyombo vya moto kuwa makini barabarani kwa kuzingatia sheria
za alama za barabara ikiwemo kuendesha vyombo hivyo kwa mwendo
unaotakiwa ili kudhibiti ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.
Kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara
ya Dodoma- Babati yenye urefu wa KM 188.1, Waziri Prof. Mbarawa amesema
kuwa barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwakani kwani kwa sasa ipo
katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
“Kazi inaenda kwa kasi kubwa,
matumaini yangu ni kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, barabara hii
itakamilika kwa viwango bora tulivyokubaliana kwenye mkataba”,
amesisitiza Profesa Mbarawa.
Amefafanua kuwa kukamilika kwa
barabara hiyo kutapunguza umbali wa masaa kwa abiria wanaosafiri kupitia
njia ya Singida wanaotoka Dodoma na mikoa ya jirani kuelekea Manyara,
Moshi na Arusha.
Ameongeza kuwa barabara hiyo
itasaidia kuiunganisha Tanzania na Nchi za kutoka Kusini na Kaskazini
mwa bara la Afrika, hivyo kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi na
kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya utalii.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala
wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu,
amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kusimamia ujenzi wa barabara hiyo
kwa viwago vinavyostahili na kuahidi kukamilika kwa wakati.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments :
Post a Comment